Qatar Airways

Fursa za Kazi Sekta ya Usafiri wa Anga (Airport Services)

Shirika la ndege la Qatar Airways linatangaza nafasi mpya za kazi kwa watu wenye shauku ya kutoa huduma bora viwanja vya ndege. Angalia nafasi hapa chini na utume maombi yako:


1. Airport Services Agent

Nafasi hii ni kwa ajili ya kutoa huduma kwa abiria kuanzia wanapoingia uwanja wa ndege (Check-in), kusaidia kwenye mageti ya kupandia ndege, na kuhakikisha safari za abiria zinaenda vizuri bila usumbufu.

  • Kuwasaidia abiria wakati wa kuwasili na kuondoka.
  • Kuhakikisha usalama na kanuni za shirika zinafuatwa.
  • Uwezo mzuri wa mawasiliano (English is mandatory).

2. Senior Airport Services Agent

Hii ni nafasi ya ngazi ya juu inayohitaji uzoefu zaidi. Utasimamia timu ya watoa huduma, kuhakikisha operesheni za kila siku za uwanja wa ndege zinafanyika kwa ufanisi wa hali ya juu na kutatua changamoto za kiutendaji.

  • Uongozi na usimamizi wa timu ya chini.
  • Kutatua matatizo magumu ya abiria kwa weledi.
  • Uzoefu wa awali katika huduma za uwanja wa ndege (Ground Handling).

Going Places Together | Qatar Airways Careers

Post a Comment

0 Comments