TANGAZO: Orodha Mpya ya Majina ya Walioitwa Kazini (Placement) – Januari 2026 (Tangazo Na. 89)

 

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetoa orodha nyingine kubwa ya majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi. Tangazo hili (Na. 89) linahusu wasailiwa waliofanya usaili katika kipindi cha kuanzia tarehe 04 Januari 2025 hadi tarehe 22 Desemba 2025.

Orodha hii pia inajumuisha waombaji waliokuwa kwenye kanzidata (Database) ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi mpya kupatikana katika mamlaka mbalimbali.

Mamlaka za Ajira na Vituo Vilivyohusika:

Tangazo hili ni pana na linajumuisha halmashauri na taasisi nyingi nchini, zikiwemo:

Halmashauri ya Manispaa ya Moshi

Halmashauri ya Mji wa Bunda

Halmashauri ya Mji wa Njombe

Halmashauri ya Wilaya ya Hai

Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua

Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa

(Na halmashauri nyingine nyingi kama zilivyoainishwa kwenye faili la PDF)

Kada Zilizoitwa Kazini:

Kada mbalimbali zimeguswa katika awamu hii, ikiwa ni pamoja na:

Sekta ya Afya: Madaktari, Wauguzi, Wafamasia, Maafisa Afya Mazingira, na Wasaidizi wa Afya.

Sekta ya Elimu: Walimu wa masomo ya Sayansi (Kemia, Fizikia, Baiolojia), TEHAMA, Biashara, na Uchumi.

Utawala na Maendeleo: Maafisa Biashara, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii, na Maafisa Sheria.

Sekta ya Uzalishaji: Maafisa Kilimo, Mifugo, Uvuvi, na Misitu.

Maelekezo Muhimu kwa Waliochaguliwa:

Kupata Barua: Barua za kupangiwa vituo vya kazi zinapatikana kupitia akaunti ya muombaji kwenye Ajira Portal. Ingia kwenye mfumo, nenda sehemu ya 'My Applications', kisha pakua (download) na uchape (print) barua yako.

Kuripoti Kazini: Unatakiwa kwenda kuripoti kwenye kituo ulichopangiwa ndani ya muda ulioainishwa kwenye barua hiyo.

Vihakiki: Hakikisha unakwenda na Vyeti Halisi (Original Certificates) kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vikahakikiwe na mwajiri kabla ya kuanza taratibu za ajira.

Jinsi ya Kuangalia Orodha Kamili:

Kuangalia kama jina lako lipo, unaweza kupakua faili kamili la PDF lenye kurasa 96 kupitia kiungo hapa chini:

👉 Bofya Hapa Kusoma Majina Yote (PDF Na. 89)

Zingatia: Ikiwa jina lako halipo kwenye orodha hii, usikate tamaa. Sekretarieti ya Ajira inaendelea kutoa matokeo ya usaili kadiri mchakato unavyokamilika. Endelea kufuatilia matangazo yanayokuja.

Hongera sana kwa wote walioitwa kazini!

Post a Comment

0 Comments