TANGAZO: Orodha ya Majina ya Vijana Waliochaguliwa Mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeship) 2025/2026 - Ofisi ya Waziri Mkuu

 

Habari Njema kwa Vijana!

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imetangaza rasmi orodha ya majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeship Training) kwa mwaka wa masomo 2025/2026.

Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za serikali katika kukuza ujuzi kwa nguvu kazi ya taifa, kusaidia vijana kupata uzoefu wa vitendo maeneo ya kazi, na kuongeza nafasi zao za kuajiriwa au kujiajiri.

Umechukuliwa? Jinsi ya Kuangalia Jina Lako

Kama uliomba nafasi hizi, sasa unaweza kukagua kama jina lako limejumuishwa kwenye orodha rasmi. Orodha hii inajumuisha vijana kutoka mikoa mbalimbali na fani tofauti za ufundi na utaalamu.

Bonyeza link hapa chini kusoma na kupakua (Download) orodha kamili ya majina:

👉 DOWNLOAD ORODHA YA MAJINA HAPA (PDF)

Maelekezo Muhimu kwa Waliochaguliwa:

Vituo vya Mafunzo: Hakikisha unajua kituo ulichopangiwa (VETA au vyuo vingine vya washirika).

Tarehe ya Kuripoti: Zingatia tarehe zilizopangwa kwa ajili ya kuanza mafunzo ili usipoteze nafasi yako.

Nyaraka Muhimu: Unapokwenda kuripoti, hakikisha una vyeti vyako halisi (Original Certificates), kitambulisho cha Taifa (NIDA), na vifaa vingine vilivyoainishwa kwenye tangazo.

Kuhusu Mafunzo ya Uanagenzi

Programu hii inalenga kuwapatia vijana ujuzi wa kiufundi katika nyanja mbalimbali kama vile:

Ujenzi na Uselemala

Ufundi wa Magari na Mitambo

Teknolojia ya Habari (TEHAMA)

Hoteli na Utalii

Na fani nyingine nyingi.

Usisahau Kushare!

Mfahamishe na mwenzako kwa ku-share post hii kwenye WhatsApp, Facebook, na Twitter ili asipitwe na fursa hii muhimu.

Kila la kheri kwa vijana wote waliochaguliwa!

Post a Comment

0 Comments