TAYARI!: Majina Mapya ya Walioitwa Kazini Utumishi (Batch 83) - January 15, 2026 | Pakua PDF Hapa

Habari njema kwa waombaji kazi!

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetoa tangazo jipya la kuitwa kazini leo, tarehe 15 Januari 2026. Hii ni orodha mpya (Batch 83) ya vijana waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi katika taasisi mbalimbali za Serikali.

Kama ulifanya usaili hivi karibuni au umekuwa ukisubiri majina kutoka kwenye Database ya Utumishi, hii ndio nafasi yako ya kuangalia kama jina lako lipo.

📌 Taarifa Muhimu za Tangazo Hili:

Tarehe ya Tangazo: 15 Januari 2026

Mtoa Tangazo: Sekretarieti ya Ajira (PSRS)

Aina ya Tangazo: Kuitwa Kazini (Placement)

Kumbukumbu Namba: TANGAZO LA KUITWA KAZINI 83

📋 Nini cha Kufanya Ukiona Jina Lako?

Kwa mujibu wa utaratibu wa Sekretarieti ya Ajira, waombaji wote walioitwa kazini wanatakiwa kuzingatia yafuatayo:

Kupata Barua ya Ajira: Ingia kwenye akaunti yako ya Ajira Portal na uangalie sehemu ya "My Applications" ili kupakua barua yako ya kupangiwa kituo.

Kuripoti Kazini: Zingatia tarehe uliyopewa kwenye barua kuripoti kwa mwajiri wako mpya.

Vyeti Halisi: Hakikisha unaenda na vyeti vyako halisi (Original Certificates) vya masomo kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki.

📥 Jinsi ya Kupata Orodha ya Majina (PDF)

Usihangaike kutafuta mbali. Tumekuwellkea Link ya moja kwa moja kupakua faili hilo la PDF lenye orodha kamili ya majina hayo.

Bofya maandishi yaliyo hapa chini kusoma majina:

👉 BONYEZA HAPA KUPAKUA PDF YA WALIOITWA KAZINI (BATCH 83)

(Kumbuka: Faili hili ni kubwa, hakikisha una bando la kutosha kulifungua)

📢 Usipitwe na Taarifa!

Jiunge na familia yetu ili uwe wa kwanza kupata nafasi mpya za kazi na matangazo ya kuitwa kazini kila yanapotoka.

Share habari hii kwa marafiki na magroup ya WhatsApp ili na wao waangalie majina yao.

Hongera sana kwa wote waliofanikiwa kuitwa kazini! 🇹🇿

Post a Comment

0 Comments