Habari njema kwa waombaji kazi wote! Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa hivi karibuni. Ikiwa uliomba nafasi za kazi UDOM kupitia Mfumo wa Ajira Portal, huu ndio muda wako wa kujiandaa kikamilifu kufanya usaili na kutimiza ndoto zako.
Tafadhali soma kwa makini maelekezo haya muhimu ili usikose fursa hii adhimu.
📅 Muda na Tarehe ya Usaili:
Usaili utafanyika kuanzia tarehe 26/02/2026 hadi 28/02/2026. (Muda na sehemu utaainishwa kwa kila kada).
⚠️ MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WASAILIWA WOTE
Ili kuruhusiwa kufanya usaili, kila msailiwa LAZIMA azingatie masharti yafuatayo:
Vifaa vya Kujikinga: Kila msailiwa anapaswa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask).
Vitambulisho: Ni lazima kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. (Vitambulisho vinavyokubalika ni: Kitambulisho cha NIDA, Mpiga kura, Kazi, Uraia, Hati ya kusafiria (Passport), Leseni ya Udereva, au Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji).
Vyeti Halisi (Original Certificates): Hakikisha unakuja na VYETI VYAO HALISI (Cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Shahada n.k).
❌ MAELEKEZO MAKALI: 'Testimonials', 'Provisional Results', 'Statement of results', na 'Result slips' HAVITAKUBALIWA NA HAUTARUHUSIWA KUFUANYA USAILI.
Vyeti vya Bodi za Kitaaluma: Kwa kada zinazohitaji usajili, njoo na vyeti halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
Mavazi na Gharama: Kila msailiwa ajigharamie Chakula, Usafiri, na Malazi. Pia, hakikisha unahudhuria ukiwa na mavazi nadhifu na yenye staha.
Vyeti vya Nje ya Nchi: Waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Mamlaka husika (TCU, NACTVET au NECTA). Waliosoma nje wanapaswa pia kuwasilisha Cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.
Tofauti ya Majina: Kama majina yako yanatofautiana kwenye nyaraka zako, unapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
BONYEZA HAPA KUPATA PDF YA MAJINA
💻 JINSI YA KUANGALIA MAJINA NA KUPATA NAMBA YAKO YA USAILI (NAMNA YA KU-APPLY TENA/KUFUATILIA)
Kwa kuwa majina haya yanatolewa kupitia mfumo rasmi wa Serikali, huna haja ya kuhangaika. Fuata hatua hizi rahisi kuona taarifa zako:
Ingia Kwenye Akaunti Yako: Nenda kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira (Ajira Portal) kupitia portal.ajira.go.tz.
Weka Taarifa Zako (Log In): Tumia Barua pepe (Email) na Nywila (Password) ulizotumia wakati wa kuomba kazi. (Kumbuka: Msailiwa anatakiwa kukumbuka password yake ili kuweza kuingia kwenye mtandao wakati wa usaili wa mchujo).
Angalia Namba ya Usaili: Wasailiwa wote walioitwa wanatakiwa kuingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya usaili. Namba hii ni muhimu sana!
Kwa Ambao Hawakuitwa: Kama hujaona jina lako, usiwe na wasiwasi. Ingia kwenye akaunti yako ya 'Ajira Portal' na utaona sababu za kutokuitwa kwako ili ufanyie kazi mapungufu hayo na usikose fursa wakati mwingine.
✨ KUMBUKA: Kujiandaa mapema ndio siri ya ushindi. Tunawatakia kila la kheri waombaji wote katika usaili wenu!
Pata Updates Zote za Ajira Kiganjani Mwako!
Usikubali kupitwa na fursa za ajira na elimu kila siku.
👉 Tembelea kurasa zetu:
📱 Facebook, Instagram & TikTok: @Upsten Ajira portal
📺 YouTube: Upsten Tv
Tafadhali sambaza (Share) ujumbe huu kwa ndugu, jamaa, na marafiki ili wajipatie taarifa hizi muhimu. Usisahau kuweka maoni yako hapa chini kama una swali lolote!

0 Comments