Habari njema kwa waombaji kazi wote! Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza rasmi matokeo ya usaili wa kuandika kwa ajili ya nafasi mbalimbali katika Chuo Kikuu Mzumbe. Usaili huu ulifanyika hivi karibuni, tarehe 19 Februari 2026.Kama wewe ni mmoja wa vijana walioshiriki katika usaili huu, huu ndio wakati sahihi wa kujua hatima yako na kujiandaa na hatua inayofuata. Karibu upate taarifa kamili na miongozo yote muhimu hapa kwenye Upsten Ajira Portal.
Maelekezo Muhimu Sana kwa Wasailiwa Wote:
Kwa wale wote ambao majina yao yametoka na kuchaguliwa kuendelea na hatua inayofuata ya usaili, Sekretarieti ya Ajira imetoa maelekezo yafuatayo ambayo ni lazima kuyafuata:
Zingatia Muda na Eneo: Wasailiwa wote wanatakiwa kuzingatia kikamilifu muda na eneo la usaili walilopangiwa. Kuchelewa kunaweza kukugharimu nafasi yako.
Nyaraka Muhimu na Kitambulisho: Ni LAZIMA kila msailiwa afike na vyeti vyake halisi (Original Certificates). Pia, usisahau kubeba Kitambulisho chako halali (kama vile NIDA, Pasi ya Kusafiria, au Leseni) kwa ajili ya utambuzi. Hakuna msailiwa atakayeruhusiwa kufanya usaili bila nyaraka hizi muhimu.
Orodha ya Kada Zilizotolewa Matokeo:
Matokeo yaliyotoka yanahusisha kada za Ukufunzi Msaidizi (Tutorial Assistants - TA) katika fani zifuatazo:
TA Accounting and Finance (Uhasibu na Fedha)
TA Environmental Management (Usimamizi wa Mazingira)
TA Logistic and Supply Chain Management (Usimamizi wa Ugavi)
TA Economics (Uchumi)
TA Production and Operational Management (Usimamizi wa Uzalishaji na Uendeshaji)
TA Agribusiness (Biashara ya Kilimo)
TA Youth Development and Leadership (Maendeleo na Uongozi wa Vijana)
Namna ya Kupakua (Kudownload) Matokeo:
Ili kurahisisha zoezi lako la kutafuta majina, tumekuunganishia matokeo ya kada zote kwenye faili moja ili uweze kupakua kwa urahisi.
BONYEZA KUPATA PDF YA MATOKEO YOTE
Bofya link hiyo hapo juu, na faili la PDF litajipakua (download) moja kwa moja kwenye simu au kompyuta yako. Fungua faili hilo, tafuta jina lako pamoja na namba yako ya mtihani, kisha angalia ratiba yako ya usaili unaofuata.
Tunawatakia kila la kheri wasailiwa wote waliofaulu kuelekea hatua ya mahojiano! Endelea kuwa nasi kupata taarifa za haraka na uhakika kuhusu fursa za ajira. Usisahau kusambaza (share) makala hii kwa ndugu na marafiki ili nao wasipitwe na fursa hii.
0 Comments