Hatimaye habari njema ambayo maelfu ya waombaji kazi mliokuwa mkiingoja imewasili! Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza rasmi leo orodha ya majina ya wasailiwa (Call for Interview) kwa ajili ya taasisi mbalimbali za Serikali.Kama uliomba nafasi ya kazi kupitia Ajira Portal hivi karibuni, huu ni wakati wako wa kuhakiki jina lako na kuanza maandalizi ya usaili utakaofanyika mwezi huu wa Machi 2026.
Orodha ya Kada Zilizotajwa Kwenye Tangazo la Leo
Tangazo hili limehusisha kada nyingi muhimu nchini, ambapo wasailiwa wamepangwa kulingana na fani zao. Kada hizo ni pamoja na:
Walimu wa Arts: Kwa ajili ya shule za Sekondari na Msingi kote nchini.
Afisa Kilimo: Wataalamu wa ugani na usimamizi wa mazao.
Maendeleo ya Jamii: Maafisa watakaohudumu katika halmashauri na taasisi mbalimbali.
Ustawi wa Jamii: Wataalamu wa huduma za kijamii na ustawi.
Mifugo: Maafisa mifugo na wataalamu wa afya ya wanyama.
Kada Zinginezo: Orodha hii pia inajumuisha kada mbalimbali za ufundi, utawala, na afya.
Maelekezo Muhimu Kuhusu Usaili wa Machi 2026
Ni muhimu kila msailiwa kusoma maelekezo yaliyomo kwenye PDF ili kutopoteza sifa za kuendelea na hatua inayofuata. Kumbuka mambo haya:
Tarehe ya Usaili: Usaili unatarajiwa kuanza rasmi ndani ya mwezi Machi 2026. Hakikisha unajua siku na saa ya kada yako.
Vitu vya Kubeba: Fika na vyeti halisi (Original Certificates) vya kitaaluma na cheti cha kuzaliwa. Pia, hakikisha una Kitambulisho cha NIDA au kitambulisho kingine rasmi.
Eneo la Usaili: Hakiki kituo chako cha usaili kwani vituo vinaweza kutofautiana (Dodoma, Dar es Salaam, au kanda nyingine).
Jinsi ya Kupata na Kupakua Majina Yote
Tumekurahisishia kazi! Badala ya kuhangaika kutafuta kila PDF peke yake, tumeyaunganisha maelekezo yote na mafaili yote manne (4) yaliyotolewa leo kwenye link moja ya uhakika.
Bofya hapa chini kupata orodha kamili na maelezo ya usaili:
👉 PAKUA MAJINA YA USAILI UTUMISHI MACHI 2026 (PDF 4)
Ushauri kwa Wasailiwa
Usaili wa Utumishi unahitaji utulivu na maandalizi ya kutosha. Pitia muongozo wa kada yako, fanya mazoezi ya maswali ya kawaida ya usaili (Oral/Aptitude), na hakikisha unafika kituoni angalau nusu saa kabla ya muda uliopangwa.
Kumbuka: Huduma za Sekretarieti ya Ajira ni bure. Epuka matapeli wanaoweza kukuomba fedha kwa ahadi ya kukusaidia kupata kazi.
Kila la kheri kwa wasailiwa wote!
0 Comments