Je, wewe ni mtaalamu wa Rasilimali Watu (HR) au Mhasibu mwenye uzoefu na unatafuta fursa mpya ya ajira jijini Dar es Salaam?
Wakala wa ajira wa Vipawa Works, moja ya makampuni yanayokua kwa kasi katika kuunganisha wataalamu na fursa za kazi nchini Tanzania, imetangaza nafasi za kazi 20 kwa ajili ya kujazwa mara moja (Immediate positions). Hii ni fursa adhimu kwa vijana na wataalamu wenye uzoefu kuingia kwenye soko la ajira kupitia wakala makini.
Kuhusu Vipawa Works
Vipawa Works ni kampuni ya uajiri iliyopo katika jengo la Alpha Plaza (lililokuwa likijulikana kama Jangid Plaza), Mbuyuni, ghorofa ya 3, ofisi namba 303, barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es Salaam. Wanafanya kazi ya kutafuta na kuchuja vipaji bora kwa ajili ya makampuni mbalimbali nchini.
Zifuatazo ni nafasi zilizotangazwa:
1. Maofisa Rasilimali Watu (Human Resources Officers) – Nafasi 10
Kampuni inatafuta Maofisa HR wenye uwezo wa kusimamia mahusiano ya wafanyakazi, uajiri, na mifumo ya utendaji kazi.
Idadi ya Nafasi: 10
Uzoefu: Miaka 3 na kuendelea katika fani ya HR.
Mahali: Dar es Salaam.
Sifa za Ziada: Mwombaji awe na uelewa mpana wa Sheria za Kazi Tanzania (Labour Laws), uwezo wa kusimamia migogoro, na ustadi wa mawasiliano.
2. Wahasibu (Accountants) – Nafasi 10
Nafasi hizi ni kwa ajili ya watu wenye umakini wa hali ya juu kwenye takwimu na ripoti za kifedha.
Idadi ya Nafasi: 10
Uzoefu: Miaka 2 na kuendelea, hususan katika uandaaji wa ripoti za kifedha (Financial Report Preparation).
Mahali: Dar es Salaam.
Sifa za Ziada: Ujuzi wa kutumia programu za kihasibu (Accounting softwares), uelewa wa masuala ya kodi (TRA/VAT), na uwezo wa kufanya uchambuzi wa kifedha.
Jinsi ya Kutuma Maombi (How to Apply)
Ikiwa unakidhi sifa zilizotajwa hapo juu, tafadhali tuma wasifu wako (CV) kwa njia ya barua pepe (Email).
Barua Pepe (Email): cv@vipawaworks.com
Mwisho wa Kutuma Maombi: Tarehe 10 Machi 2026.
Mawasiliano kwa Maelezo Zaidi:
Ikiwa una changamoto au unahitaji ufafanuzi zaidi, unaweza kuwasiliana na Vipawa Works kupitia:
Simu (Call): 0757 888110
WhatsApp: 0717 443616
Ofisi: Alpha Plaza, Ghorofa ya 3, Ofisi Na. 303, Mbuyuni, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Muhimu Kuzingatia:
Hakikisha CV yako imesasishwa (Updated) na inaonyesha uzoefu unaohitajika.
Unapofanya maombi, weka kichwa cha habari cha barua pepe (Subject line) kulingana na nafasi unayoomba (mfano: APPLICATION FOR ACCOUNTANT POSITION).
Maombi yote ni lazima yafike kabla ya tarehe 10 Machi 2026.
Usisahau kushea fursa hii na marafiki au ndugu zako wanaotafuta kazi jijini Dar es Salaam. Kila la heri katika maombi yako!
0 Comments