NAFASI ZA KAZI 2026: The Islamic Foundation Inatafuta Watangazaji na Wasimamizi wa Vipindi (Programmes)

Taasisi mashuhuri ya The Islamic Foundation (TIF), yenye makao makuu yake mkoani Morogoro, imetangaza fursa mpya za ajira kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi katika tasnia ya habari na utangazaji. Taasisi hii, inayojulikana kwa kutoa huduma za kijamii na kidini, inalenga kuimarisha kitengo chake cha habari kwa kuajiri wataalamu wenye weledi.

Kama wewe ni mwanahabari unayetafuta mazingira ya kazi yanayozingatia maadili, nidhamu, na weledi wa hali ya juu, hizi hapa ni nafasi zilizotangazwa:

1. Presenter / Mtangazaji (Nafasi 02)

Nafasi hizi ni kwa ajili ya watu wenye vipaji vya utangazaji na uwezo wa kuwasiliana vyema na hadhira.

Sifa za Kitaaluma: Mwombaji lazima awe na Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) katika fani ya Mass Communication.

Uzoefu: Inahitajika kuwa na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili (2 years) katika fani husika.

2. Program Director (Nafasi 01)

Mkurugenzi wa Vipindi atakuwa na jukumu la kusimamia maudhui na ubunifu wa programu mbalimbali.

Sifa za Kitaaluma: Shahada ya Kwanza katika mojawapo ya fani zifuatazo: Mass Communication, Media Studies, Broadcasting, au Journalism.

Uzoefu: Lazima uwe umefanya kazi kwa angalau miaka miwili (2 years) katika nafasi inayohusiana na usimamizi wa maudhui ya habari.

3. Program Controller (Nafasi 01)

Huyu ni msimamizi mkuu wa mtiririko wa vipindi ili kuhakikisha kila kitu kinatekelezwa kulingana na ratiba na viwango vya taasisi.

Sifa za Kitaaluma: Shahada ya Kwanza katika Mass Communication, Media Studies, Broadcasting, au Journalism.

Uzoefu: Uzoefu wa kazi wa miaka miwili (2 years) unahitajika.

Sifa ya Ziada (Adding Advantage)

Kwa waombaji wote, kuwa na Elimu ya Dini (Religious Education) itakuwa ni sifa ya ziada itakayompa mwombaji nafasi nzuri zaidi ya kufikiriwa.

Jinsi ya Kutuma Maombi (Mode of Application)

Ikiwa una vigezo vilivyotajwa hapo juu, unakaribishwa kutuma maombi yako kwa njia mbili:

Kwa Barua Pepe (Email): Tuma wasifu wako (CV) na barua ya maombi kwenda: hro@islamicftz.org.

Kwa Njia ya Posta: Tuma maombi yako kwa anuani ifuatayo:

Chairman,

The Islamic Foundation,

P.O. Box 6011,

Morogoro.

Kwa maswali au ufafanuzi zaidi, unaweza kuwasiliana na ofisi kupitia namba: +255 626 42 6930.



Post a Comment

0 Comments