NAFASI ZA KAZI 96: HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE (MARCH 2026

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika manispaa hiyo kuomba nafasi za kazi za mkataba. Tangazo hili limetolewa rasmi tarehe 09/03/2026 likiwa na kumbukumbu namba TMC/MD/B.2/37/118.
Fursa hizi zinajumuisha Kada ya Afya na kada zingine muhimu kwa maendeleo ya manispaa.
Mchanganuo wa Nafasi na Sifa za Kitaaluma

 * Muuguzi II (Nafasi 34): Mwombaji awe na Stashahada (Diploma) ya uuguzi kutoka chuo kinachotambuliwa na kusajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

 * Mhudumu wa Afya (Nafasi 21): Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne na kupata mafunzo ya mwaka mmoja katika fani ya afya.

 * Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja II (Nafasi 10): Mwombaji awe na Stashahada (Diploma) ya Uuguzi na awe amesajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga.

 * Mteknolojia Maabara (Nafasi 09): Mwombaji awe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia na awe amesajiliwa na mabaraza yanayohusika.

 * Afisa Muuguzi II (Nafasi 06): Mwombaji awe na Shahada ya Uuguzi, amehitimu mafunzo ya vitendo (Internship), na kusajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

 * Mteknolojia Dawa (Nafasi 06): Mwombaji awe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia na kusajiliwa na mabaraza husika.

 * Tabibu Anastezia (Nafasi 03): Mwombaji awe mhitimu wa Kidato cha Nne/Sita mwenye Stashahada ya Tabibu.

 * Mfamasia (Nafasi 02): Mwombaji awe na Shahada ya Famasi, amehitimu mafunzo ya vitendo (Internship) ya mwaka mmoja, na kusajiliwa na Baraza la Famasi.

 * Mteknolojia Mionzi (Nafasi 02): Mwombaji awe na Stashahada ya Uteknolojia na kusajiliwa na mabaraza husika.

 * Tabibu (Nafasi 02): Mwombaji awe mhitimu wa Kidato cha Nne/Sita mwenye Stashahada (Diploma) ya Tabibu.

 * Mhasibu (Nafasi 01): Mwombaji awe na Shahada ya Biashara/Sanaa yenye mwelekeo wa Uhasibu, Stashahada ya juu ya Uhasibu (Advanced Diploma), au Intermediate Certificate kutoka NBAA, pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu.
Masharti ya Jumla kwa Waombaji

 * Uraia na Umri: Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 na 45.

 * Vithibitisho vya Vyeti: Vyeti vyote vya taaluma na cheti cha kuzaliwa lazima vithibitishwe (Certified) na Mwanasheria au Wakili.

 * Hati za Matokeo: Hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (Result Slips) hazitakubaliwa.

 * Maelezo Binafsi (CV): Ambatisha CV inayojitosheleza yenye anwani, namba za simu, na majina ya wadhamini watatu.

 * Leseni za Kazi: Kazi zote zinazohitaji leseni, waombaji lazima waambatishe nakala za leseni zao.

 * Vyeti vya Nje: Waliostudoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimeidhinishwa na TCU, NECTA, au NACTE.

 * Watumishi wa Umma: Waombaji ambao tayari ni waajiriwa katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Maombi yote yaandikwe kwa mkono au kuchapwa na yatumwe kwa njia ya barua kwenda kwa:
Mkurugenzi Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,
S.L.P 46343,
DAR ES SALAAM.
📅 Mwisho wa kutuma maombi: Tarehe 20/03/2026 saa 9:30 alasiri.
Imetolewa na:
Jomaaly Satura
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke.

Post a Comment

0 Comments