UPSTEN AJIRA PORTAL
TANGAZO LA KUITWA KAZINI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote waliofanya usaili katika nafasi mbalimbali kuwa matokeo ya waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.
Waombaji wote waliofaulu usaili wanatakiwa kupakua barua zao za kupangiwa vituo vya kazi kupitia akaunti zao za Ajira Portal (My Applications) na kwenda kuripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya muda uliopangwa.
Aidha, waombaji wanatakiwa kufika na vyeti halisi (Original Certificates) kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa ajira rasmi.

0 Comments