TANGAZO MAALUM: Majina ya Walioitwa Kazini MUHAS (Aprili 2026)

Habari njema kwa waombaji kazi wote! Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ametoa tangazo rasmi la kuwaita kazini waombaji wote waliofaulu usaili uliofanyika kati ya tarehe 17 Februari 2026 na 18 Februari 2026.

Kama ulishiriki katika usaili huu wa nafasi mbalimbali za kitaaluma (kama vile Wakufunzi, Watafiti, na Wakutubi), huu ndio wakati wa kufuatilia matokeo yako. Uongozi umesisitiza kuwa wale ambao majina yao hayapo kwenye tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi, hivyo wasikate tamaa na waendelee kuomba pindi nafasi zingine zitakapotangazwa.

📌 Mambo Muhimu ya Kuzingatia kwa Waliofaulu:

Wale wote waliobahatika kuwepo kwenye orodha wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo kikamilifu:

Muda wa Kuripoti: Unatakiwa kuripoti kwa Mwajiri ndani ya siku saba (7) kuanzia tarehe 08 Aprili, 2026.

Nyaraka Zinazohitajika: Siku unayoripoti lazima uwe na nyaraka hizi halisi (Originals) ili zihakikiwe kabla ya kupewa barua ya ajira:

Vyeti vya masomo kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea (O-Level, A-Level, Degree, n.k).

Kitambulisho cha Taifa au Namba ya NIDA.

Cheti cha Kuzaliwa (Birth Certificate).

👥 Baadhi ya Kada Zilizotangazwa:

Tangazo hili linajumuisha jumla ya waombaji 20 walioitwa kwenye kada mbalimbali zikiwemo:

Lecturer (PhD) – Pharmaceutical Microbiology

Assistant Research Fellow – Epidemiology and Biostatistics

Assistant Lecturer – Community Health & Biostatistics

Tutorial Assistants – Katika idara za Anaesthesia, Orthopaedics, Nursing, Dentistry, Optometry, Paediatrics n.k.

Assistant Librarian Trainee.

(Je, jina lako limo kwenye orodha hii? Soma maelekezo hapo chini ili kuweza kupakua faili lenye majina yote).

📥 NAMNA YA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA:

Ili kuona orodha kamili ya majina 20 ya waombaji wote walioitwa kazini na kusoma tangazo hili kwa kina, unaweza kudownload faili la PDF kwa urahisi kabisa.

Jinsi ya kupakua (Download):

Bofya link iliyoangaziwa hapo chini.

Faili la PDF litafunguka au kuanza kujipakua moja kwa moja kwenye simu/kompyuta yako.

Fungua faili hilo kwenye sehemu ya "Downloads" kwenye kifaa chako ili kusoma majina.

👉 BOFYA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO LA KUITWA KAZINI MUHAS

Tunawatakia kila la kheri wale wote waliofanikiwa kupata ajira hii mpya!

Post a Comment

0 Comments