Tangazo la Kuitwa Kazini 2026: Majina ya Walioitwa Kazi na Vituo vya Kazi | Ajira Portal

Tangazo la Kuitwa Kazini - Ajira 2026

Tangazo la Kuitwa Kazini – Waombaji Waliofaulu Usaili

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametoa tangazo la kuitwa kazini kwa waombaji mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 11-08-2025 na 07-05-2026.

Tangazo linahusisha pia baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Nafasi za Kazi na Vituo vya Kazi

  • Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa – Daktari Daraja la II (Medical Officer Grade II).
  • Halmashauri ya Mji Nanyamba – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Halmashauri ya Mji Newala – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kyela – Mteknolojia Dawa Daraja II (Technologist Pharmacy Grade II).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Makete – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara – Afisa Kilimo Msaidizi Daraja la II, Afisa Maendeleo ya Jamii Daraja II, Katibu wa Kamati Daraja la II, Msaidizi wa Afya Daraja la I na Mwalimu Daraja la IIIA.
  • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba – Afisa Kilimo Msaidizi Daraja la II, Afisa Mifugo Msaidizi Daraja la II, Msaidizi wa Afya Daraja la I, Msaidizi wa Afya Daraja la II, Mwalimu Daraja la III B, Mwalimu Daraja la III B – Shule ya Msingi, Mwalimu Daraja la IIIA na Tabibu Daraja la II (Clinical Officer Grade II).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea – Mwalimu Daraja la III C, Historia ya Tanzania na Maadili, pamoja na Mwalimu Daraja la III C – Kiswahili.
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Newala – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Tarime – Mwalimu Daraja la III C, Historia ya Tanzania na Maadili.
  • Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe – Mwalimu Daraja la III C, Somo la Biashara (Business Studies).
  • Shirika la Masoko ya Kariakoo (KMC) – Technician II (Electrical).

Masharti na Taarifa Muhimu

  • Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi watapata barua zao za kupangiwa vituo vya kazi kupitia akaunti zao za Ajira Portal katika sehemu ya My Applications.
  • Waombaji wanatakiwa kupakua na kuchapisha barua zao za kupangiwa vituo vya kazi na kwenda nazo wakati wa kuripoti katika vituo walivyopangiwa.
  • Walioitwa kazini wanatakiwa kuripoti kwa mwajiri ndani ya muda ulioainishwa kwenye barua zao za kupangiwa kituo cha kazi.
  • Wakati wa kuripoti wanatakiwa kuwa na vyeti halisi vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki wa mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
  • Waombaji ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili, na wanashauriwa kuomba tena nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Tarehe ya Tangazo

Tangazo limetolewa tarehe 19-08-2026.

Pakua Tangazo Kamili

Pakua PDF Hapa

Post a Comment

0 Comments