Nafasi za Kazi MOFAT: Madereva wa Basi 200 na Maafisa Huduma kwa Abiria (PSO) 160
Kuhusu MOFAT
MOFAT ni kampuni inayojitambulisha kama "Your Trusted Business Partner". Kampuni inawakaribisha wananchi kujiunga na timu yake ili kuwa sehemu ya usafiri salama, wa kisasa na unaowaunganisha watu wa Dar es Salaam. Maadili yake ni Jamii Salama, Huduma Bora na Kesho Iliyo Bora. Kauli mbiu yake ni "Kazi Tofauti, Lengo Moja: Kuwasogeza Watu Mbele".
Nafasi za Kazi
1. Dereva wa Basi (Nafasi 200)
Majukumu makuu
- Kuendesha mabasi ya BRT kwa usalama na uwajibikaji.
- Kuhakikisha usalama na faraja ya abiria.
- Kuzingatia sheria za barabarani na sera za kampuni.
- Kudumisha usafi na hali nzuri ya basi.
- Kutoa huduma bora kwa wateja.
Sifa za mwombaji
- Leseni ya udereva Daraja C (magari makubwa).
- Cheti cha PSV (Veta/NIT).
- Cheti cha BRT (NIT).
- Uzoefu wa kuendesha angalau miaka 3.
- Umri kati ya miaka 25 hadi 50.
2. Afisa Huduma kwa Abiria (PSO) (Nafasi 160)
Majukumu makuu
- Kuwahudumia abiria kwenye vituo na ndani ya basi.
- Kutoa taarifa sahihi za safari.
- Kusaidia upandaji na ushushaji wa abiria, na usimamizi wa foleni.
- Kuhakikisha mazingira salama, yenye utaratibu na rafiki.
- Kuwakilisha MOFAT kwa weledi na ukarimu.
Sifa za mwombaji
- Elimu ya kidato cha nne (Form Four) au zaidi.
- Uwezo mzuri wa mawasiliano na mahusiano na watu.
- Uzoefu wa huduma kwa wateja ni faida zaidi.
- Muonekano wa heshima na tabia ya kitaalamu.
Masharti na Taarifa Nyingine Muhimu
- Maombi yanatumwa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya MOFAT.
- Mwombaji anatakiwa kukidhi sifa zilizoainishwa kwa nafasi anayoomba.
Mawasiliano na maelezo zaidi:
- Simu: +255 759 777 444
- Tovuti: mofat.co.tz
- Anwani: Peninsula Noble Center, Msasani, Dar es Salaam
Tarehe ya Mwisho ya Maombi
05 Oktoba 2026

0 Comments