Nafasi 8 za Kazi Dereva Daraja II – Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
Kuhusu Taasisi
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, chini ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Mkurugenzi Mtendaji wake, inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 8, kama ilivyoainishwa katika tangazo lenye kumbukumbu namba KUMB.NA.HW/S.20/54/104 la tarehe 05 Oktoba, 2026.
Nafasi za Kazi na Sifa Zinazohitajika
Dereva Daraja II (Driver II) – Nafasi 8
Majukumu ya kazi:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kufanya usafi wa gari.
Sifa za mwombaji:
- Awe na cheti cha kidato cha Nne (Form IV).
- Awe na leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyompatia sifa ya kupata madaraja husika.
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Ngazi ya mshahara: TGS B
Masharti na Taarifa Nyingine Muhimu
- Waombaji wote wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45. Kwa nafasi za ndani ya taasisi za kijeshi: waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi miaka 25, na waombaji wa nafasi za shahada wasizidi miaka 30.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji walioajiriwa katika Utumishi wa Umma WASIOMBE, na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo binafsi (CV), na nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ikiwemo vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika (Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates) pamoja na vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards).
- "Testimonials", "Provisional Results", "Statement of results" na hati za matokeo za kidato cha nne na sita (Form IV and Form VI results slips) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa kada zinazohitaji GPA waliosoma nje ya Tanzania, waambatishe cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba, isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Wahusika watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
- Barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa iambatishwe pamoja na vyeti vya elimu, na anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, S.L.P 355, Tanga.
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani: https://portal.ajira.go.tz/
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
- Waombaji wote wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira unazingatia misingi ya haki, usawa na uwazi.
Tarehe ya Mwisho ya Maombi
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 18 Oktoba, 2026.

0 Comments