Nafasi 63 za Kazi Kafiti Foundation (NGO) - Mwanza (January 2026)

Shirika la Kafiti Foundation (Non-Governmental Organization) linalojishughulisha na maendeleo ya jamii, linatangaza nafasi 63 za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo. Nafasi hizi zimegawanyika katika ajira za muda mrefu (Long-Term) na ajira za muda mfupi (Short-Term).
Hii ni fursa nzuri kwa wakazi wa Mwanza, hususan Wilaya ya Ilemela, kujiunga na timu inayolenga kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia uwezeshaji wa kiuchumi, elimu, na afya.

1. Ajira za Muda Mrefu (Long-Term Positions)

Nafasi hizi ni kwa ajili ya kuendesha shughuli za kila siku za ofisi na miradi ya shirika.
Nafasi Zinazohitajika:
Project Manager
Administrative Assistant
Communication Officer / Public Relations (PR)
Monitoring and Evaluation (M&E) Officer
Secretary / Customer Service Officer
Graphic Designer
Photographer / Photo Shoot Officer
Transport Officer (Bodaboda) - Lazima awe na leseni hai.
Drivers (Nafasi 2) - Lazima awe na leseni hai.
Office Cleaner
Cook
Security Guard - Lazima awe na mafunzo rasmi ya ulinzi (Kipaumbele kwa wakazi wa Kata ya Kahama).
Mahali pa Kazi: Kafiti Foundation HQ, Magaka Road, Kahama, Wilaya ya Ilemela, Mwanza.

2. Ajira za Muda Mfupi (Short-Term Positions - 50 Posts)

Nafasi hizi ni kwa ajili ya kukusanya na kuingiza takwimu katika kata zote 19 na mitaa 171 ya Wilaya ya Ilemela.
Nafasi Zinazohitajika:

Data Collectors (Nafasi 46)
Data Entry Clerks (Nafasi 4)
Sifa za Waombaji (Data Collectors & Clerks):
Elimu: Kidato cha Nne, Cheti, au Diploma.
Awe mkazi wa Wilaya ya Ilemela na anaufahamu vizuri mtaa au kata anayoomba.
Awe na nidhamu, umakini, na uwezo mzuri wa mawasiliano.
Uzoefu wa kutumia Google Forms na kumiliki Smartphone ni sifa ya ziada.
Awe tayari kufanya kazi "Full-time" kwa muda wa mradi.

Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao yakiwa na viambatanisho vifuatavyo:
CV (Wasifu) yenye mawasiliano.
Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
Barua fupi ya maombi.
Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa (Kwa nafasi za muda mfupi).

Njia za Kutuma:
Barua Pepe (Email): info@kafitifoundation.org
Fika Ofisini: Kafiti Foundation HQ, Magaka Road, Kahama, Ilemela, Mwanza.
Mwisho wa Kutuma Maombi:
Tarehe: 06 Februari 2026
Zingatia:

Andika jina la nafasi unayoomba kwenye kichwa cha barua pepe au bahasha.
Hakuna malipo yoyote yanayohitajika wakati wa usaili.





Post a Comment

0 Comments