Je, unatafuta kazi Serikalini? Habari njema ni kwamba Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza fursa mpya za ajira kwa mwaka 2026 kupitia Mfumo wa Ajira Portal. Hii ni nafasi ya kipekee kwa wahitimu na wataalamu mbalimbali kujiunga na utumishi wa umma.Katika post hii, utapata maelezo kamili kuhusu nafasi hizi, sifa zinazohitajika, na mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutuma maombi yako bila kukosea.
🏢 Kuhusu Ajira Portal
Ajira Portal ni mfumo rasmi wa Serikali unaosimamiwa na Sekretarieti ya Ajira (PSRS) chini ya Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Mfumo huu unahakikisha mchakato wa ajira unakuwa wa wazi, haki, na unaozingatia sifa.
📋 Mahali pa Kupata Matangazo ya Kazi
Matangazo yote mapya ya kazi huwekwa katika tovuti rasmi ya Ajira. Ili kuona nafasi zilizotangazwa hivi punde (PDF files), tembelea: www.ajira.go.tz.
Hapo utaweza kupakua matangazo na kusoma sifa za kila nafasi kabla ya kutuma maombi.
✅ Sifa na Mahitaji Muhimu
Kabla ya kuanza kuomba, hakikisha una vitu vifuatavyo:
Vyeti vya Taaluma: Vyeti vyote (Form IV, VI, Chuo) lazima viwe vimehakikiwa (Certified) na Wakili au Hakimu.
Barua ya Maombi: Iandikwe kwa Kiingereza au Kiswahili kulingana na maelekezo ya tangazo.
Wasifu (CV): Iwe imejitosheleza na kuonyesha uzoefu wako.
Picha: Picha ya hivi karibuni (Passport size).
Cheti cha Kuzaliwa: Nakala iliyohakikiwa.
🚀 Jinsi ya Kutuma Maombi (Hatua kwa Hatua)
Kutuma maombi kupitia Ajira Portal ni rahisi ukifuata hatua hizi:
Tembelea Mfumo: Ingia katika tovuti ya maombi: portal.ajira.go.tz.
Jisajili (Register): Kama huna akaunti, bofya "Register" kutengeneza akaunti mpya. Kama unayo, bofya "Login".
Jaza Taarifa Zako (My Profile): Hakikisha umejaza sehemu zote kikamilifu (Taarifa binafsi, Elimu, Uzoefu wa kazi, nk).
Pakia Viambatanisho (Attachments): Upload vyeti vyako vyote vilivyohakikiwa (Certified copies), CV, na barua ya maombi.
Tafuta Kazi: Nenda kwenye sehemu ya "Job Vacancies", chagua kazi unayotaka kuomba.
Tuma Maombi: Bofya kitufe cha “Apply Now”. Hakikisha unapokea ujumbe wa uthibitisho kuwa maombi yako yametumwa.
⚠️ Zingatia Haya (Muhimu Sana!)
Usitoe Rushwa: Huduma za Ajira Portal ni BURE. Usilipe pesa kwa mtu yeyote ili kupata kazi.
Wahi Mapema: Usisubiri siku ya mwisho (deadline) ndio utume maombi ili kuepuka msongamano wa mtandao.
Usahihi wa Taarifa: Hakikisha majina yako kwenye akaunti yanafanana na yale yaliyo kwenye vyeti vyako.
📅 Mwisho wa Kutuma Maombi:
Tarehe za mwisho hutofautiana kulingana na kila tangazo la kazi (Soma PDF husika kwa umakini).
Share post hii na marafiki zako ili wasipitwe na fursa hii! Kazi Ipo, Jipange!
0 Comments