ORODHA YA NAFASI MPYA ZA KAZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) – 2026

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetangaza fursa mbalimbali za ajira kwa Watanzania wenye sifa na vigezo stahiki. Hii ni fursa adhimu kwa wataalamu wa kada tofauti kujiunga na taasisi hii kongwe na yenye heshima kubwa nchini.

Nafasi hizi nyingi zipo chini ya miradi na vituo mbalimbali vya chuo, ikiwemo Kituo cha Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabianchi (Centre for Climate Change Studies - CCCS).

Orodha ya Nafasi Zilizotangazwa:

Hapa chini ni orodha ya nafasi wazi zinazohitaji kujazwa kwa sasa:

1. Programme Officer

2. TPP Program Officer

3. Monitoring and Evaluation Officer

4. Project Officer

5. Office Assistant

Sifa za Jumla na Vigezo (Qualifications):

Kwa kuwa nafasi ni tofauti, sifa zinazohitajika zinatofautiana kulingana na aina ya kazi.

Kazi za ofisini (kama Office Assistant) zinahitaji elimu kuanzia ngazi ya Cheti/Diploma.

Kazi za kitaalamu na usimamizi wa miradi zinahitaji elimu ya kuanzia Shahada ya Kwanza (Bachelor's Degree), Shahada ya Uzamili (Master's), hadi Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani husika.

Mwisho wa Kutuma Maombi:

Mwisho wa kupokea maombi kwa nafasi nyingi kati ya hizi ni tarehe 26 Februari, 2026. Tunashauri kutuma maombi yako mapema iwezekanavyo.

Jinsi ya Kusoma Maelezo Kamili na Kutuma Maombi:

Ili kusoma maelezo ya kina (Job Description) ya kila nafasi na kutuma maombi yako moja kwa moja kwenye mfumo rasmi wa ajira wa UDSM, tafadhali bonyeza link hapa chini.

NAMNA YA KUPATA NAFASI ZA KAZI UDSM (MWONGOZO WA HARAKA)

Wasomaji wengi wamekuwa wakikutana na changamoto ya kuona ujumbe wa "0 Vacancy" wanapofungua link ya UDSM. Hii inatokea kwa sababu mfumo unakupeleka kwenye kitengo kimoja tu (kama Auxiliary Police).

Ili kuona nafasi zingine zote (kama Programme Officer, Office Assistant, n.k.), fuata hatua hizi rahisi:

Hatua za Kufuata:

Fungua Link Rasmi: Bonyeza link ya maombi iliyopo hapa chini.

Shuka Chini Kabisa: Ukurasa utakapofunguka, usishtuke ukiona "0 Vacancy". Shuka (scroll) chini kabisa ya ukurasa huo.

Tafuta Nafasi Husika: Chini utazikuta nafasi zote zilizoorodheshwa zikiwa na maelezo yake na kitufe cha "Apply Now".

👉 Bofya hapa kufika kwenye ukurasa wa kazi:

Zingatia: Hakikisha unawahi kutuma maombi yako kabla ya tarehe 26 Februari, 2026

Post a Comment

0 Comments