Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Programme - WFP) nchini Tanzania limetangaza nafasi ya mafunzo kwa vitendo (Internship) kwa vijana wenye sifa katika kitengo cha usimamizi wa miradi na uratibu.
Maelezo ya Nafasi:
Nafasi: Intern (Project Management and Coordination Support)
Kitambulisho cha Kazi (Job ID): JR113993
Kituo cha Kazi: Dar es Salaam, Tanzania
Hali ya Tangazo: Re-Advertisement (Limerudiwa)
Majukumu makuu:
Kusaidia katika uratibu wa miradi mbalimbali ya shirika.
Kukusanya na kuchakata takwimu za miradi.
Kusaidia katika maandalizi ya ripoti na mikutano ya kiofisi.
Kufanya kazi kwa karibu na timu ya usimamizi ili kuhakikisha malengo ya shirika yanafikiwa.
Sifa za Mwombaji:
Awe amehitimu au yuko katika hatua za mwisho za masomo ya Shahada (Bachelor's Degree) katika fani zinazohusiana na Usimamizi wa Miradi, Maendeleo ya Jamii, Uchumi, au Biashara.
Uwezo mzuri wa kuwasiliana kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili.
Ujuzi wa kutumia kompyuta (MS Office).
Jinsi ya Kuomba:
Maombi yote yanatumwa moja kwa moja kupitia mfumo wa ajira wa WFP (Workday). Unaweza kupata link ya kutuma maombi hapa:
Mwisho wa Kutuma Maombi: Tafadhali tembelea link hiyo haraka iwezekanavyo kwani nafasi huchukuliwa mapema.
0 Comments