Ajira Namtumbo Agosti 2026: Nafasi 6 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo – Agosti 2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ametangaza nafasi za kazi sita (06) kwa Watanzania wenye sifa, baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Nafasi za Kazi na Sifa Zinazohitajika

1. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 04

Kazi na Majukumu:

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
  • Kupokea wageni na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
  • Kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba nyingine za kazi.
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
  • Kupokea majalada na kuyasambaza kwa Maofisa walio katika Idara, Kitengo au Sehemu husika.
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

Sifa za Mwombaji:

  • Awe amehitimu Kidato cha Nne.
  • Awe na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili.
  • Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa maneno 100 kwa dakika moja.
  • Awe na ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi kama vile Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS C

2. Dereva Daraja la II – Nafasi 02

Kazi na Majukumu:

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kufanya usafi wa gari.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.

Sifa za Mwombaji:

  • Awe na cheti cha Kidato cha Nne.
  • Awe na leseni ya Daraja C au E ya uendeshaji magari.
  • Awe amefanya kazi ya udereva kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
  • Awe na vyeti vya mafunzo vilivyompatia sifa ya kupata madaraja husika.
  • Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS B

Masharti ya Jumla

  • Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha aina ya ulemavu wao kwenye mfumo wa kuombea.
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detailed Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana, anuani ya barua pepe pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  • Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na hati za matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (Results Slips) hazitakubaliwa.
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wawe na kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Waombaji wa nafasi ya Dereva Daraja la II wenye leseni Daraja C na E wanapaswa kuambatisha vyeti vya mafunzo ya udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi utasababisha wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
  • Ni waombaji watakaokidhi sifa zinazotakiwa pekee ndio watakaoitwa kwenye usaili.

Anuani ya Barua ya Maombi

Barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu inapaswa kuelekezwa kwa:

Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo,
2 Barabara ya Boma,
S.L.P 55,
57382 NAMTUMBO.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

APPLY NOW

Tarehe ya Mwisho ya Maombi

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 24 Agosti 2026.

Pakua Tangazo Kamili

Pakua PDF Hapa

Tangazo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.

Post a Comment

0 Comments