Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Songwe 2026 - Dereva na Mwandishi Mwendesha Ofisi

Tangazo la Nafasi za Kazi - Halmashauri ya Wilaya ya Songwe

Kumb. Na.: SDC/C.30/45/35
Tarehe: 31 Agosti 2026

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi tano (5) katika Halmashauri hii, baada ya kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

1. Dereva Daraja la II - Nafasi Nne (4)

Sifa za Kuajiriwa

Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Majukumu na Kazi

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  • Kufanya usafi wa gari.
  • Kufanya kazi zingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

Ngazi ya Mshahara

TGS B

2. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II - Nafasi Moja (1)

Sifa za Kuajiriwa

Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) pamoja na Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja, na awe amepata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email na Publisher.

Majukumu na Kazi

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
  • Kusaidia kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaelekeza sehemu wanazoweza kushughulikiwa.
  • Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anayofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
  • Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
  • Kusaidia kufikisha maelezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na kumtaarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
  • Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
  • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.

Ngazi ya Mshahara

TGS C

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  • Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao, kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa kuambatisha vyeti vya mafunzo ya udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detailed Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail Address), pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe, na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika: Diploma/Certificates, Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV na VI, Computer Certificate, na Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards).
  • Testimonial, Provisional Results, Statement of Results, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (Form IV and Form VI results slips) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, ikielekezwa kwa: Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, S.L.P 77, Songwe.
  • Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa "Recruitment Portal".

Tarehe ya Mwisho ya Maombi

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 13 Septemba, 2026.

Limetolewa na: Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya ya Songwe

Pakua PDF Hapa

Post a Comment

0 Comments