Kuitwa Kwenye Usaili - Tume ya Utumishi wa Mahakama (TUMA) Septemba 2026

Kuitwa Kwenye Usaili wa Awali - Tume ya Utumishi wa Mahakama (TUMA)

Septemba 14, 2026, Dodoma

Tume ya Utumishi wa Mahakama (Judiciary Service Commission) ni chombo cha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachosimamia masuala ya ajira na utumishi ndani ya Mahakama.

Taarifa ya Usaili

Kufuatia Tangazo la nafasi za ajira lililotolewa na Tume ya Utumishi wa Mahakama tarehe 14 Agosti, 2026, waombaji wa nafasi za ajira katika kada mbalimbali wanafahamishwa kuwa, baada ya kukamilika kwa zoezi la uchambuzi wa maombi, waombaji waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wa hatua ya kwanza watafanya usaili kuanzia tarehe 22 Septemba, 2026 hadi 24 Septemba, 2026, katika muda na vituo vilivyoonyeshwa kwenye orodha ya majina ya wasailiwa iliyoambatishwa na Tangazo hili.

Usaili wa hatua ya kwanza utafanyika kwa njia ya mtandao (Kielektroniki) kwa kila kada iliyoainishwa kwenye jedwali, kwa tarehe husika kuanzia saa 2:00 asubuhi. Hivyo, wasailiwa wanapaswa kufika kwenye kituo cha usaili saa 1:30 asubuhi.

Ratiba ya Usaili wa Kwanza

Na. Tarehe Siku Kada
1 22 Septemba, 2026 Jumanne Afisa Hesabu II
Msaidizi wa Hesabu II
2 23 Septemba, 2026 Jumatano Hakimu Mkazi II
Mwandishi Mwendesha Ofisi II
Msaidizi wa Ofisi
4 24 Septemba, 2026 Alhamisi Msaidizi wa Kumbukumbu II

Masharti na Maelekezo kwa Wasailiwa

  • Kila msailiwa anatakiwa kuwa na kitambulisho halali chenye picha kinachotambulika na Serikali. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Hati ya kusafiria, Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura au Leseni ya Udereva.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu na Shahada kutegemeana na sifa za nafasi husika. Nakala za vyeti hazitakubaliwa na ambao hawatakuwa na vyeti vyao halisi hawaruhusiwi kufanya usaili.
  • Kwa wasailiwa waliosoma nje ya Tanzania wawasilishe uthibitisho wa uhakikiwa wa vyeti vyao na Mamlaka husika (TCU, NACTVET au NECTA).
  • Kila msailiwa anapaswa kuhudhuria usaili akiwa na mavazi nadhifu na yenye staha. Aidha, kila msailiwa atajigharamia Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Nyaraka zifuatazo hazitakubalika na msailiwa atakayewasilisha hataruhusiwa kuendelea na usaili: Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form IV and form VI results slips).
  • Wasailiwa wote wanatakiwa kukumbuka anuani zao za barua pepe (email address) na nywila (password) walizotumia wakati wa kuwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (ajira.jsc.go.tz). Kushindwa kukumbuka taarifa hizo kutamzuia kufanya usaili.
  • Kila msailiwa atapaswa kufanya usaili katika kituo alichopangiwa.
  • Wasailiwa watakaofaulu usaili wa hatua ya kwanza watafahamishwa kuhusu tarehe, muda na utaratibu wa hatua inayofuata ya usaili, ambayo inaweza kuwa Usaili wa Mdomo (Oral Interview) na/au Usaili wa Vitendo (Practical Interview), kupitia tovuti ya Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Mawasiliano Zaidi

Kwa maulizo zaidi piga simu Na. 0734219821 au 0738247341 au tuma barua pepe: maulizo.ajira@jsc.go.tz

Imetolewa na:
Lydia Churi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Tume ya Utumishi wa Mahakama

Pakua PDF Hapa

Post a Comment

0 Comments