Nafasi za Kazi PPRA 2026: ICT Officer II (Frontend, Backend, AI, Systems Analyst) - Ajira Tanzania

Nafasi za Kazi PPRA (ICT Officer II) - Public Service Recruitment Secretariat

Ref. Na. JA.9/16/01/54  |  Tarehe: 01 Septemba, 2026

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), kwa niaba ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), inatangaza nafasi kumi (10) za kazi kwa Watanzania wenye sifa, weledi, uadilifu na uwezo wa kujituma katika fani mbalimbali za TEHAMA.

1. ICT Officer II (Software Development – Frontend) - Nafasi 3

Majukumu

  • Kushiriki katika uchambuzi, ubunifu, uendelezaji, upimaji, uwekaji na matengenezo ya programu za wavuti na simu zenye usalama na urahisi wa matumizi;
  • Kuendeleza miundo ya programu za wavuti kwa kutumia Angular, TypeScript, HTML5, Tailwind CSS na mbinu za kisasa za CSS;
  • Kuendeleza na kudumisha programu za simu za mkononi (cross-platform) kwa kutumia Flutter na Dart, ikijumuisha uchapishaji kupitia Google Play Console na Apple App Store;
  • Kuunganisha programu za mbele (frontend) na simu na REST APIs, GraphQL na miundo mingine ya mifumo ya taasisi;
  • Kushiriki katika upimaji, urekebishaji, uboreshaji wa utendaji na usimamizi wa msimbo kupitia Git; na
  • Kuandaa nyaraka za kiufundi na majukumu mengine kama atakavyoelekezwa na msimamizi.

Sifa na Uzoefu

Shahada ya Kwanza katika Sayansi ya Kompyuta, Uhandisi wa Programu, Teknolojia ya Habari, Mifumo ya Habari, Uhandisi wa Kompyuta au sifa nyingine inayolingana kutoka chuo kinachotambulika. Mwombaji anatakiwa awe na uzoefu wa vitendo au portfolio ya uendelezaji wa programu, ikiwa ni pamoja na: uzoefu wa Angular v14+ (au Vue.js, React, Svelte akiwa tayari kujifunza Angular); umahiri wa TypeScript, programu za object-oriented na reactive; Tailwind CSS, HTML5, Flexbox, CSS Grid na Angular Material; uzoefu wa Flutter na Dart pamoja na usimamizi wa state kama NgRx; uzoefu wa uchapishaji programu Google Play Console na Apple App Store; uzoefu wa REST APIs na GraphQL (Apollo Client au GraphQL Flutter); umahiri wa Git, GitHub au GitLab. Ujuzi wa Figma utakuwa ni fursa ya ziada.

Ngazi ya Mshahara: PPRA 5

2. ICT Officer II (Software Development – Backend) - Nafasi 4

Majukumu

  • Kushiriki katika uchambuzi, ubunifu, uendelezaji, upimaji na matengenezo ya mifumo ya nyuma (backend), huduma za wavuti na microservices zenye usalama na uwezo wa kupanuka;
  • Kuendeleza huduma za backend kwa kutumia Java na Spring Boot, ikijumuisha RESTful APIs na GraphQL; kuunganisha mifumo ya ndani na nje kwa kutumia Spring Cloud OpenFeign, APIs na RabbitMQ;
  • Kubuni na kuboresha hifadhidata za PostgreSQL kwa kutumia SQL, indexing, Spring Data JPA na Hibernate; kutekeleza usalama wa backend kwa kutumia Spring Security, OAuth2, JWT, Redis, JUnit, Testcontainers, Swagger/OpenAPI na Postman; na kutumia Git, CI/CD na mazingira ya containerization; na
  • Kutekeleza majukumu mengine kama atakavyoelekezwa na msimamizi.

Sifa na Uzoefu

Shahada ya Kwanza katika Sayansi ya Kompyuta, Uhandisi wa Programu, Teknolojia ya Habari, Mifumo ya Habari au Uhandisi wa Kompyuta kutoka chuo kinachotambulika. Mwombaji anatakiwa awe na uzoefu wa vitendo au portfolio ya uendelezaji wa programu, ikiwa ni pamoja na: umahiri wa Java 21 au zaidi; uendelezaji wa backend kwa Spring Boot, Spring Data JPA na Hibernate; uzoefu wa REST APIs, GraphQL, Spring Cloud OpenFeign, PostgreSQL, RabbitMQ, usindikaji wa asynchronous, event-driven architecture, Git na CI/CD ya msingi. Ujuzi wa Kubernetes, Redis, Spring Security, OAuth2, JWT, JUnit 5, GraphiQL na Postman utakuwa ni fursa ya ziada.

Ngazi ya Mshahara: PPRA 5

3. ICT Officer II (Artificial Intelligence Applications) - Nafasi 2

Majukumu

  • Kushiriki katika uchambuzi, ubunifu, uendelezaji, upimaji na matengenezo ya programu za Akili Bandia (AI), ikijumuisha uunganishaji na programu za wavuti na simu;
  • Kuendeleza scripts za backend, mifumo ya utekelezaji wa AI, RESTful APIs na huduma za asynchronous kwa kutumia Python, TypeScript au JavaScript;
  • Kusanidi, kuweka na kudumisha Large Language Models (LLM) za ndani kwa kutumia Ollama, LM Studio, vLLM au LocalAI, pamoja na LLM APIs za mtandaoni kama OpenAI, Gemini au Anthropic;
  • Kubuni prompts madhubuti na kutekeleza matokeo ya AI yaliyopangwa kwa kutumia JSON schemas, function calling na tool use;
  • Kuendeleza mifumo ya agentic AI na Retrieval-Augmented Generation (RAG) kwa kutumia embeddings, vector similarity search na vector databases; na
  • Kutumia Git na deployment pipelines, kuandaa nyaraka za kiufundi na majukumu mengine kama atakavyoelekezwa.

Sifa na Uzoefu

Shahada ya Kwanza katika Sayansi ya Kompyuta, Uhandisi wa Programu, Akili Bandia, Sayansi ya Takwimu (Data Science) au fani nyingine ya kiufundi inayohusiana kutoka chuo kinachotambulika. Mwombaji anatakiwa awe na uzoefu wa vitendo au portfolio ya kiufundi, ikiwa ni pamoja na: umahiri wa Python, TypeScript au JavaScript kwa scripting ya backend, mifumo ya utekelezaji wa AI, uunganishaji wa RESTful API na JSON; umahiri wa Git, GitHub au GitLab; uzoefu wa kusanidi LLM za ndani (Ollama, LM Studio, vLLM, LocalAI) au LLM APIs za mtandaoni (OpenAI, Gemini, Anthropic), ikijumuisha prompt engineering, structured outputs, JSON schemas na function calling. Ujuzi wa agentic AI workflows, LangChain, LlamaIndex, AutoGPT, embeddings, vector databases (Chroma, Qdrant, Pinecone), RAG na uunganishaji wa AI na Angular, React au Flutter utakuwa ni fursa ya ziada.

Ngazi ya Mshahara: PPRA 5

4. ICT Officer II (Systems Analyst) - Nafasi 1

Majukumu

  • Kushiriki katika uchambuzi wa mifumo, uchambuzi wa michakato ya biashara na ukusanyaji wa mahitaji ya mifumo ya habari;
  • Kuandaa vipimo vya mfumo, nyaraka za kiufundi na miongozo ya watumiaji;
  • Kushiriki katika upimaji, uwekaji, matengenezo na uboreshaji endelevu wa mifumo ya habari;
  • Kutoa msaada wa kiufundi kwa watumiaji na kushiriki katika mafunzo na uhamasishaji;
  • Kushiriki katika uboreshaji wa michakato ya biashara na miradi ya mageuzi ya kidijitali;
  • Kushiriki katika uchambuzi wa takwimu, uunganishaji wa mifumo na shughuli za udhibiti wa ubora;
  • Kufuatilia utendaji wa mfumo na kupendekeza uboreshaji unaofaa; na
  • Kutekeleza majukumu mengine kama atakavyoelekezwa na msimamizi.

Sifa na Uzoefu

Shahada ya Kwanza katika Sayansi ya Kompyuta, Mifumo ya Habari, Teknolojia ya Habari, Uhandisi wa Programu, Uhandisi wa Kompyuta, Mifumo ya Habari za Biashara au sifa nyingine inayolingana kutoka chuo kinachotambulika. Mwombaji lazima awe na ujuzi au uzoefu wa vitendo katika uchambuzi wa mifumo, mifumo ya habari ya taasisi, ukusanyaji wa mahitaji ya watumiaji, upimaji wa mfumo, msaada wa kiufundi kwa watumiaji, uchambuzi wa michakato ya biashara na uandaaji wa nyaraka za kiufundi. Ujuzi wa usalama wa mtandao (cyber security), programu za taasisi na mifumo ya TEHAMA ya Serikali utakuwa ni fursa ya ziada.

Ngazi ya Mshahara: PPRA 5

Masharti ya Jumla

  • Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45.
  • Waombaji waombe kwa kuzingatia taarifa zilizotolewa katika tangazo hili.
  • Waombaji lazima waambatishe nakala zilizohakikiwa za: Vyeti vya Shahada/Stashahada/Astashahada/Cheti; Transcript za Shahada/Stashahada/Astashahada; Vyeti vya Usajili wa Kitaaluma na Mafunzo kutoka Mabaraza husika (pale inapohitajika); na Cheti cha kuzaliwa.
  • Haitakubalika kuambatisha: Vyeti vya matokeo ya Kidato cha Nne na Sita; Testimonial na transcript pungufu.
  • Mwombaji lazima apakie Picha ya Passport mpya kwenye Mfumo wa Ajira.
  • Watumishi walio katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba; wanapaswa kuzingatia Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Mstaafu wa Utumishi wa Umma kwa sababu yoyote ile hatakiwi kuomba.
  • Mwombaji aoneshe wadhamini watatu waaminifu wenye mawasiliano ya uhakika.
  • Vyeti vyote vya kitaaluma vya kigeni LAZIMA vitambuliwe na Mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTVET). Waombaji wa nafasi zenye masharti ya GPA LAZIMA waambatishe cheti cha mahesabu ya GPA kutoka TCU.
  • Barua ya maombi iliyosainiwa iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza na kuelekezwa kwa: Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, S.L.P 2320, Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, Dodoma.
  • Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) pekee. Maombi yatakayotumwa kwa njia nyingine yoyote hayatapokelewa.
  • Wagombea watakaoitwa usaili pekee ndio watakaojulishwa tarehe ya usaili.
  • Uwasilishaji wa vyeti feki au taarifa za uongo utachukuliwa hatua za kisheria.

Tarehe ya Mwisho ya Maombi

14 Septemba, 2026

Pakua PDF Hapa

Post a Comment

0 Comments