Majina Walioitwa Kwenye Usaili 17 Oktoba – 11 Novemba 2026 | Sekretarieti ya Ajira (PDF)

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili – Tarehe 05 Oktoba, 2026 (Sekretarieti ya Ajira)

Kumb. Na. JA.9/16/01/59 – Tarehe 05/10/2026

Kuhusu Tangazo

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya waajiri mbalimbali, anawataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 17/10/2026 hadi 11/11/2026. Baada ya usaili, waombaji watakaofaulu watapangiwa vituo vya kazi.

Baadhi ya waajiri wanaohusika ni Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Shirika la Posta Tanzania (TPC), Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Orodha kamili ya waajiri iko kwenye PDF.

Ratiba ya Usaili (Mifano Tu)

Ratiba ina aina nne za usaili: Usaili wa Mchujo, Usaili wa Vitendo, Usaili wa Mahojiano na Usaili wa Alama za Barabarani. Chini ni mifano michache tu. Ratiba kamili na majina ya waitwa usaili yako kwenye PDF.

Aina ya UsailiMwajiriKadaTarehe na MudaMahali
MchujoHospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)Artisan II (Plumber)17/10/2026, saa 1:00 asubuhiKwa njia ya mtandao (Online)
MchujoWizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na MichezoICT Officer Grade II – Developer17/10/2026, saa 1:00 asubuhiKwa njia ya mtandao (Online)
VitendoTume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)Plant Operator II19/10/2026, saa 1:00 asubuhiOfisi za Makao Makuu ya Tume, Njedengwa – Dodoma
VitendoChuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)Artisan II (Carpentry)19/10/2026, saa 1:00 asubuhiUDSM – Utawala
MahojianoTume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)Quantity Surveyor II20/10/2026, saa 1:00 asubuhiOfisi za Sekretarieti ya Ajira (PSRS), Tambukareli, Mtaa wa Mahakama – Dodoma
Alama za BarabaraniShirika la Posta Tanzania (TPC)Driver II19/10/2026, saa 1:00 asubuhiVETA Buza – Dar es Salaam
Alama za BarabaraniChuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)Driver II19/10/2026, saa 1:00 asubuhiChuo cha VETA Kihonda – Morogoro

Yapi ya Kuangalia Kwenye PDF

  • Ratiba kamili ya kila aina ya usaili: Mchujo, Vitendo, Mahojiano na Alama za Barabarani.
  • Majina ya waitwa usaili, yaliyopangwa kwa mwajiri na kada, pamoja na tarehe na mahali pa usaili.
  • Kwa usaili wa mchujo wa mtandaoni, kituo cha usaili kitatangazwa kupitia akaunti yako ya "Ajira Portal" na tovuti ya Sekretarieti ya Ajira (www.ajira.go.tz).
  • Ukiwa hujaona jina lako kwenye tangazo, ingia kwenye akaunti yako ya Ajira Portal kuona sababu za kutokuitwa.

Masharti na Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa

  • Fika kwenye eneo la usaili ukiwa umevaa barakoa (mask).
  • Kuwa na kitambulisho cha utambuzi, kama Kitambulisho cha Mkazi, Mpiga Kura, Kazi, Uraia, Hati ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji.
  • Fika na vyeti halisi, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kulingana na sifa za nafasi husika.
  • Testimonials, Provisional Results, Statement of Results na hati za matokeo za kidato cha IV na VI (result slips) havitakubaliwa, na mwenye hati hizo hataruhusiwa kuendelea na usaili.
  • Kada zinazosajiliwa na Bodi za Kitaaluma zinatakiwa kuja na vyeti halisi vya usajili na leseni za kufanyia kazi.
  • Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi, na ahudhurie usaili akiwa na mavazi nadhifu na yenye staha kulingana na Waraka wa mavazi.
  • Waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na mamlaka husika (TCU, NACTVET au NECTA). Kwa kada zinazohitaji GPA, wawasilishe cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.
  • Ingia kwenye akaunti yako na unakili namba ya usaili. Wanaofanya usaili wa mchujo kwa mtandao wakumbuke barua pepe na nywila wanazotumia kwenye Ajira Portal.
  • Wenye majina yanayotofautiana kwenye nyaraka zao wawasilishe Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
  • Ni marufuku kutoa au kupokea rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi.

Tarehe ya Usaili

Usaili utafanyika kuanzia tarehe 17/10/2026 hadi 11/11/2026.

Pakua PDF Hapa


Post a Comment

0 Comments