Mabadiliko Mapya ya Mitaala ya Elimu Tanzania 2025: Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo
Maboresho ya mitaala yanayoendelea yanabadilisha mfumo wa elimu nchini Tanzania kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari hadi vyuo vya ualimu. Makala hii inafafanua mabadiliko makuu kama yalivyoainishwa katika taarifa hii.
1. Mitihani na Muundo Mpya
- Mtihani wa darasa la saba utafutwa ifikapo mwaka 2027.
- Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne. Hii itaitwa Elimu ya Msingi.
- Kutakuwa na Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment) ifikapo mwaka 2027.
2. Fani na Lugha ya Kufundishia
- Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza. Hii itaanzia Sekondari, ambapo kutakuwa na mikondo miwili: Jumla na Amali.
- Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa Kiswahili. Kiingereza kitakuwa kama somo kwa Shule za Kiswahili Medium, na lugha ya kufundishia English, ambapo Kiswahili kitakuwa kama somo kwa Shule za English Medium.
3. Elimu ya Awali na ya Msingi
- Elimu ya Msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.
- Elimu ya Awali: mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5. Mwanzoni elimu ya awali haikuwa rasmi na shule za Serikali haikuwepo. Sasa itakuwepo kwa utaratibu huo.
- Masomo ya Elimu ya Msingi yatakuwa: KKK (Kusoma, Kuhesabu, Kuandika), Jiografia, Kiswahili, Sanaa na Michezo, Hisabati, Sayansi, Historia ya Tanzania na Maadili, Dini, Kiingereza na Stadi za Kazi itachomekwa.
4. Lugha Shuleni na Mikondo ya Sekondari
- Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili, na Kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiingereza.
- Shule zenye uwezo zitafundisha angalau somo moja la lugha za kigeni kama Kichina au Kifaransa.
- Sekondari kutakuwa na mikondo miwili: mkondo wa Jumla na Amali (Ufundi). Mwanafunzi atachagua kulingana na uwezo na malengo yake ya baadaye.
5. Mkondo wa Amali (Ufundi)
Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani zifuatazo:
- Kilimo na Ufugaji
- Umakenika
- Biashara na Ujasiriamali
- Sanaa na Ubunifu
- Elimu ya Michezo
- Ufugaji wa Nyuki
- Uchimbaji wa Madini
- Urembo
6. Masomo na Vyeti vya Amali
- Mwanafunzi wa Mkondo wa Amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.
- Masomo ya jumla ya wanafunzi wa Amali ni:
- Hisabati
- Elimu ya Biashara
- Kiingereza
- Historia ya Tanzania na Maadili
- Wahitimu wa Amali watapata vyeti viwili, yaani Cheti cha ujumla cha Elimu ya Sekondari (NECTA) na Cheti cha Amali (NACTIVET).
7. VETA na Usimamizi wa Ufundi
- Kila shule itakuwa na Wakala wa VETA ili kusimamia masuala ya Ufundi.
- Kila shule haitakuwa na Mikondo zaidi ya miwili ya Ufundi. Hii ni kwa ajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.
- Kutaanzishwa somo jipya la Mawasiliano ya Kitaaluma (Academic Communication) katika A-level na Ualimu.
8. Masomo Mapya na Yaliyounganishwa
- Coding itafundishwa Shule za Msingi.
- Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.
- Civics itaunganishwa na Historia ya Tanzania na Maadili kwa O-level.
- O-level masomo ya lazima yatakuwa 6, badala ya 7 ya sasa.
9. Masomo ya O-level
Masomo ya O-level yatakuwa:
| Biology | Kiswahili |
| Physics | English |
| Chemistry | Elimu ya Biashara |
| History | Computer Science |
| Geography | Bible Knowledge |
| Hisabati | Historia ya Tanzania na Maadili |
| Utunzaji wa Taarifa za Fedha | Elimu ya Dini ya Kiislamu, n.k. |
10. Masomo Yaliyofutwa na Kuchagua
- Katika O-level, masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwa sababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya Jiografia na Sayansi ya Shule ya Msingi, kwa mfano Afya ya Jamii, Afya ya Uzazi, Magonjwa ambukizi, n.k.
- Civics, Maarifa ya Jamii, Uraia na Maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la Historia ya Tanzania na Maadili.
- General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la Historia ya Tanzania na Maadili na Mawasiliano ya Kitaaluma.
11. Mafunzo ya Walimu
- Astashahada ya Ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (Diploma) ya Elimu ya Awali, Ualimu wa Msingi na Ualimu wa Elimu Maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.
- Walimu wa Sekondari wote watakuwa na Shahada (Degree), kwa sababu nchi nyingi zinaenda na mwelekeo huu.
- Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa Sekondari vitatumika kutoa Continuous Professional Development.
Hitimisho
Elimu yetu, mwelekeo mpya. Hifadhi makala hii na umtumie mzazi, mwalimu au mlezi ili wote tuelewe mabadiliko haya.

0 Comments