Nafasi ya Kuhamia: Afisa Sheria Mwandamizi (Nafasi 01) – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Kumb. Na. JA.9/259/01/B/58 – Tarehe 29 Septemba 2026
Kuhusu Taasisi
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Rais, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katibu wa Sekretarieti, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais, anakaribisha maombi ya nafasi ya kuhamia kutoka kwa Watanzania walio ndani ya Utumishi wa Umma wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi moja (01) kama ilivyoainishwa hapa chini.
Nafasi ya Kazi: Afisa Sheria Mwandamizi – Nafasi 01
Majukumu ya Kazi
- Kutoa ushauri na msaada wa kisheria kwa Sekretarieti ya Ajira.
- Kutoa mapendekezo ya maboresho katika uandaaji wa miswada ya kisheria/sheria na sheria ndogo, pamoja na kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
- Kufuatilia mashauri yaliyopo Mahakamani kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
- Kusimamia uandaaji na mapitio ya nyaraka mbalimbali za kisheria.
- Kushiriki katika majadiliano na vikao mbalimbali vinavyohitaji utaalamu wa kisheria.
- Kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kushughulikia mashauri ya madai ya kiraia yanayohusisha Sekretarieti.
Sifa za Mwombaji
- Awe mtumishi wa Umma mwenye Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) kutoka katika taasisi zinazotambuliwa na Serikali.
- Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka saba (7) katika eneo linalohusiana na kazi hiyo.
- Awe amehudhuria na kufaulu mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (Internship) au Shule ya Sheria Tanzania.
- Awe amesajiliwa kama wakili wa Mahakama Kuu.
- Awe mtumishi wa Umma aliyefanya kazi kwa mwajiri wa sasa kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
- Awe tayari kujigharamia gharama za uhamisho.
Ngazi ya Mshahara
Utazingatia viwango vya mshahara vilivyoainishwa kwenye Muundo wa Maendeleo ya Utumishi wa Taasisi.
Masharti ya Jumla
- Waombaji wote wawe raia wa Tanzania ambao ni watumishi wa Umma.
- Mwombaji lazima awe mtumishi wa Umma aliyefikia ngazi ya Mwandamizi.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika, pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma na nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (kwa waliofikia kiwango hicho), vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika (Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates), na Computer Certificate.
- "Testimonials", "Provisional Results", "Statement of results" na hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI Results Slips) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET).
- Watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anwani http://portal.ajira.go.tz/. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Muhimu
Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa, iliyopitishwa na mwajiri, pamoja na vyeti vya elimu. Anwani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
MTAA WA MAHAKAMA,
ENEO LA TAMBUKARELI,
S. L. P. 2320,
DODOMA.
Tarehe ya Mwisho ya Maombi
12 Oktoba 2026

0 Comments