Nafasi 143 za Kazi za Kujitolea Kilwa DC 2026: Afisa Habari, Hesabu, Tabibu, Muuguzi, Dereva, Mlinzi na Zaidi | Mwisho 14/10/2026

Tangazo la Nafasi 143 za Kazi za Kujitolea – Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

Tarehe ya tangazo: 28 Septemba, 2026

Kumb: Na. HB.318/329/01/4

Kuhusu Taasisi

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa Halmashauri zilizo chini ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ofisi ya Waziri Mkuu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri anawatangazia Watanzania wote wenye sifa nafasi za ajira za kujitolea kama zilivyoainishwa hapa chini.

Sifa za Jumla kwa Waombaji Wote

  • Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka kumi na nane (18) na usiozidi miaka thelathini na tano (35), pia awe na Kitambulisho cha Uraia (NIDA).
  • Awe na Elimu ya Cheti cha ngazi ya Astashahada, Stashahada au Shahada kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  • Awe hajawahi kuajiriwa katika Taasisi yoyote ya Umma tangu alipohitimu masomo.
  • Awe na Wadhamini wawili (2) ambao ni Watumishi wa Umma.
  • Awe na barua ya Mtendaji wa Kijiji/Kitongoji/Serikali za Mitaa ya Utambulisho.
  • Awe na utayari wa kujitolea katika eneo husika.
  • Awe hajawahi kuhukumiwa Mahakamani kwa makosa ya jinai.
  • Awe na uwezo wa kutumia Kompyuta au simu janja (Smart phone).

Nafasi za Kazi na Sifa Zinazohitajika

Na.NafasiIdadi
1Afisa Habari II1
2Msaidizi wa Hesabu42
3Tabibu Daraja la II8
4Mtekinolojia (Radiografia) II1
5Mteknolojia (Dawa) II10
6Mteknolojia Maabara II7
7Dereva II4
8Msaidizi wa Afya10
9Afisa Manunuzi Msaidizi1
10Afisa Muuguzi Msaidizi II5
11Muuguzi II6
12Fundi Sauti1
13Fundi Mchundo II (Magari)1
14Afisa Sheria1
15Mlinzi (Security Guard)39
16Msaidizi wa Ofisi6

1. Afisa Habari II – Nafasi 1

  • Awe amehitimu na kupata Cheti cha Shahada ya Uandishi wa Habari au Mawasiliano ya Umma kutoka kwenye Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

2. Msaidizi wa Hesabu – Nafasi 42

  • Awe amehitimu Diploma ya Uhasibu, ATEC II kutoka NBAA, Certificate in Accountancy, Certificate in Accountancy and Finance, Certificate in Business Administration majoring in Accountancy, Certificate in Commerce majoring in Accountancy au Certificate in Finance.

3. Tabibu Daraja la II – Nafasi 8

  • Wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Stashahada ya Tabibu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

4. Mtekinolojia (Radiografia) II – Nafasi 1

  • Wenye Shahada ya Sayansi katika fani ya Radiolojia na ambao wamesajiliwa na Mabaraza ya taaluma hiyo.

5. Mteknolojia (Dawa) II – Nafasi 10

  • Kuajiriwa wenye Stashahada katika fani ya Uteknolojia ya Dawa kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Mabaraza ya dawa.

6. Mteknolojia Maabara II – Nafasi 7

  • Kuajiriwa wenye Stashahada katika fani ya Uteknolojia katika fani ya Maabara kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Mabaraza ya Maabara.

7. Dereva II – Nafasi 4

  • Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanya kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
  • Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

8. Msaidizi wa Afya – Nafasi 10

  • Wahitimu wa kidato cha nne wenye cheti cha mafunzo ya Msaidizi wa Afya au Fundi Sanifu Afya Mazingira kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

9. Afisa Manunuzi Msaidizi – Nafasi 1

  • Awe amehitimu stashahada ya ugavi na manunuzi na kupata cheti kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali, na awe amesajiriwa na bodi ya manunuzi (PSPTB).

10. Afisa Muuguzi Msaidizi II – Nafasi 5

  • Kuajiriwa wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

11. Muuguzi II – Nafasi 6

  • Kuajiriwa wenye cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

12. Fundi Sauti – Nafasi 1

  • Awe amehitimu Stashahada/Shahada ya Sound Engineering, Audio Engineering au fani inayohusiana na kupata cheti cha kuhitimu kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  • Awe na ujuzi wa kutumia vifaa vya sauti kama mixing console, microphone na amplifiers, speakers, DJ equipment na vifaa vingine vya sauti.

13. Fundi Mchundo II (Magari) – Nafasi 1

  • Kuajiriwa wahitimu wenye Elimu ya kidato cha nne na Cheti cha Ufundi Stadi (Trade Test Grade II/CBET II) yenye mwelekeo wa Ufundi Magari – ‘Motor Vehicle Mechanics’ kutoka VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

14. Afisa Sheria – Nafasi 1

  • Awe amehitimu shahada ya Sheria (L.L.B) na kupata cheti na amehudhuria mafunzo ya shule ya Sheria (law school).

15. Mlinzi (Security Guard) – Nafasi 39

  • Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.

16. Msaidizi wa Ofisi – Nafasi 6

  • Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne waliohudhuria mafunzo ya muda mfupi katika maeneo yafuatayo: Office Attendant Course, Office Management, Messangerial Course, Office Clerk kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Masharti na Taarifa Nyingine Muhimu

  • Muda wa kujitolea utakuwa wa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili (12) na kinaweza kuhuishwa kwa vipindi visivyozidi viwili.
  • Watalipwa Sh. 250,000/= kwa mwezi kugharamia usafiri na chakula.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono zikiwa na anwani kamili ya Mwombaji pamoja na namba ya Simu. Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa:

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
SLP 160
Kilwa Masoko

Tarehe ya Mwisho ya Kupokea Maombi

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14/10/2026 saa 9:30 Alasiri.

Hemed S. Magaro
Mkurugenzi Mtendaji (W)

Post a Comment

0 Comments