📢 JOB ADVERTISEMENT: ANDA AUTO LIMITED / SHACMAN
Kampuni ya Anda Auto Limited (Shacman) iliyopo Dar es Salaam, inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uzoefu wa kutosha kujaza nafasi zifuatazo:
1️⃣ Sales Specialists (Nafasi 7)
Majukumu ya Kazi:
Kutangaza na kuuza malori (trucks) na mitambo mizito (heavy-duty machines).
Kutafuta na kuanzisha fursa mpya za kibiashara.
Kujenga na kudumisha mahusiano mazuri na wateja.
Kufikia na kuvuka malengo ya mauzo (sales targets).
Kuandaa ripoti za mauzo na kufuatilia maoni ya wateja.
Sifa za Mwombaji:
Shahada (Bachelor) au Stashahada (Diploma) ya Sales, Marketing, Business, au fani inayohusiana.
Uzoefu wa kuanzia miaka 3 na kuendelea katika uuzaji wa malori na mitambo mizito.
Rekodi iliyothibitishwa ya mauzo kwenye sekta ya magari au mitambo.
Uwezo mkubwa wa majadiliano (negotiation) na mawasiliano.
2️⃣ Technicians (Nafasi 10)
Majukumu ya Kazi:
Kugundua hitilafu (diagnosis), kufanya matengenezo na ukarabati wa malori na mitambo mizito.
Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mitambo.
Kutambua matatizo ya kimekanika na kiumeme (mechanical & electrical faults).
Kuhakikisha ukarabati unazingatia viwango vya ubora na usalama.
Sifa za Mwombaji:
Cheti (Certificate) au Stashahada (Diploma) ya Automotive Engineering au fani inayohusiana.
Uzoefu wa kuanzia miaka 4 na kuendelea katika matengenezo ya malori.
Ujuzi wa hali ya juu katika ufundi wa malori (truck mechanics).
Uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea na chini ya shinikizo.
Jinsi ya Kuomba (How to Apply):
Kama unakidhi vigezo, tafadhali tuma CV yako na utaje nafasi unayoomba (Clear position title) kupitia njia ya WhatsApp pekee kwenda namba:
⚠️ ONYO: Ni marufuku kupiga simu (NO PHONE CALLS ALLOWED). Watakaofuzu hatua ya kwanza ndio watakaotafutwa.
📅 Mwisho wa kutuma maombi: Tarehe 9 Machi, 2026.
0 Comments