Nafasi 40 za Kazi za Mkataba: Wakusanya Mapato Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi – Machi 2026

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi anawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kutuma maombi ya kazi ya mkataba kwa ajili ya nafasi za Wakusanya Mapato (Revenue Collectors).

Nafasi hizi ni kwa ajili ya vijana wachapakazi watakaosaidia kuimarisha ukusanyaji wa mapato katika maeneo mbalimbali ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

Maelezo ya Nafasi:

Nafasi: Mkusanja Mapato (Revenue Collector)

Idadi: 40

Aina ya Kazi: Mkataba

Kituo cha Kazi: Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi (Mkoa wa Rukwa)

Sifa za Mwombaji:

Awe ni raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.

Awe na elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).

Awe na Stashahada (Diploma) au Cheti (Certificate) katika fani za Uhasibu (Accounting), Biashara (Business Administration), Fedha (Finance), au fani nyingine inayohusiana.

Awe na uwezo wa kutumia vifaa vya kielektroniki vya kukusanyia mapato (POS Machines).

Awe mwaminifu, muadilifu, na mwenye uwezo wa kufanya kazi kwa bidii chini ya usimamizi mdogo.

Majukumu ya Kazi:

Kukusanya ushuru, kodi, na ada mbalimbali za Halmashauri katika maeneo yaliyopangwa.

Kutoa stakabadhi halali za malipo kupitia mashine za POS.

Kuhakikisha fedha zote zilizokusanywa zinawasilishwa kwa wakati Benki au kwa mweka hazina.

Kutunza kumbukumbu sahihi za makusanyo ya kila siku.

Kutoa ripoti ya makusanyo kwa msimamizi wake wa kazi.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI (MODE OF APPLICATION)

Waombaji wote wanapaswa kutuma barua za maombi kwa njia ya Posta au kuziwasilisha moja kwa moja ofisini. Barua iambatane na:

Wasifu wa mwombaji (CV).

Nakala za vyeti vya elimu na taaluma.

Nakala ya cheti cha kuzaliwa.

Picha mbili (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.

Tuma maombi yako kwa:

Mkurugenzi Mtendaji (W),

Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi,

S.L.P 45,

NAMANYERE - RUKWA.

Mwisho wa Kutuma Maombi:

Tarehe 25 Machi, 2026

Post a Comment

0 Comments