Nafasi ya Kazi: Security Guard III (Askari wa Usalama III)

 Nafasi za Kazi Benki Kuu ya Tanzania (BoT) – Machi 2026

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza nafasi mpya za kazi kwa niaba ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT). BoT inatafuta vijana Watanzania wenye sifa, nidhamu na uzalendo ili kujaza nafasi za ulinzi katika taasisi hiyo muhimu nchini.

Kama wewe ni mhitimu wa JKT/JKU na unatafuta fursa ya kipekee ya kuitumikia nchi kupitia BoT, hii hapa ni nafasi yako:

Nafasi ya Kazi: Security Guard III (Askari wa Usalama III)

Idadi ya Nafasi: 13

Taasisi: Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Mshahara: BTSS 1

Sifa za Mwombaji:

Awe na Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) na ufaulu katika masomo ya Kiingereza na Kiswahili.

Awe na Cheti cha Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au JKU.

Lazima awe na daraja la “B” la tabia na uwezo wa kazi (Behaviour and Work Competence).

Mafunzo ya JKT/JKU yawe yamehitimishwa kuanzia mwaka 2023 na kuendelea.

Majukumu ya Kazi:

Kulinda mali za Benki dhidi ya wizi na vitendo vya uvunjifu wa sheria.

Kusimamia funguo za ofisi za Benki.

Kuzuia au kuwaondoa wanaokiuka taratibu za usalama kwa kutumia nguvu inapobidi.

Kutoa huduma za kusindikiza (escort) mizigo ya Benki na wafanyakazi wanaotekeleza majukumu nyeti.

Kukagua wageni wanaoingia au kutoka katika majengo ya Benki au makazi ya viongozi.

Kufanya doria (patrol) katika maeneo ya ofisi za Benki kuhakikisha usalama wa wafanyakazi na mali.

Kurekodi matukio yote katika kitabu cha matukio (Occurrence Book) kila siku.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI (MODE OF APPLICATION)

Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Sekretarieti ya Ajira (Ajira Portal). Hakikisha unapakia (upload) vyeti vyako vyote halali ikiwemo cheti cha sekondari na cheti cha JKT/JKU.

Ili kutuma maombi, bofya link iliyo hapa chini:

BOFYA HAPA KUOMBA (Apply Now)

Mwisho wa Kutuma Maombi:

Tarehe 24 Machi, 2026.

Kumbuka: Hakuna malipo yoyote yanayotakiwa wakati wa mchakato wa kuomba kazi hizi. Kuwa mwangalifu na matapeli.

Post a Comment

0 Comments