Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ametangaza nafasi za kazi 19 kwa watanzania wenye sifa baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kama unatafuta fursa ya ajira serikalini, hii hapa ni nafasi yako! Chini ni maelezo ya kina ya nafasi hizo:
1. DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 13)
Sifa za Mwombaji:
Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV).
Leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari.
Uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
Cheti cha mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) kutoka VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Mshahara: Ngazi ya TGS B.
2. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (NAFASI 6)
Sifa za Mwombaji:
Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
Stashahada (Diploma - NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
Ujuzi wa kutumia kompyuta.
Mshahara: Ngazi ya TGS C.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 na 45.
Waambatanishe Maelezo Binafsi (CV) iliyosheheni anwani, namba ya simu na barua pepe ya uhakika pamoja na majina ya wadhamini watatu.
Vyeti vyote vya taaluma na cheti cha kuzaliwa lazima vithibitishwe na Mwanasheria/Wakili (Certified copies).
Barua ya maombi inaweza kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza na ielekezwe kwa:
MKURUGENZI WA JIJI,
HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA,
S.L.P 149,
MBEYA.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Recruitment Portal unaosimamiwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kupitia anuani:
👉 https://portal.ajira.go.tz/
KUMBUKA: Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au mkono (physical) hayatafanyiwa kazi.
📅 MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: Tarehe 17 Machi, 2026.
Kila la heri kwa waombaji wote!
Shiriki habari hii na rafiki yako anayetafuta kazi!
0 Comments