TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI: Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) - Machi 2026

Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), ametoa tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa waombaji kazi walioomba nafasi mbalimbali chuoni hapo.

Usaili unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 05 Machi 2026 hadi 06 Machi 2026.

MUHTASARI WA USAILI

Mwalozi/Mwajiri: Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

Kada Inayoitwa: Tutorial Assistant - Health Information System Management

Tarehe ya Usaili wa Mchujo (Written): 05 Machi 2026 (Saa 1:00 Asubuhi)

Tarehe ya Usaili wa Mahojiano (Oral): 06 Machi 2026 (Saa 1:00 Asubuhi)

Mahali/Kituo cha Usaili: Mbeya University of Science and Technology - Nyerere Hall

MAHITAJI NA MAELEKEZO MUHIMU KWA WASAILIWA

Wasailiwa wote wanaoitwa wanapaswa kuzingatia mambo yafuatayo ili kuruhusiwa kushiriki usaili:

Vyeti Halisi (Original Certificates): Kila mshiriki lazima afike na vyeti vyake halisi kuanzia kidato cha nne, sita, Astashahada, Stashahada, Shahada na kuendelea kulingana na nafasi husika. Testimonials na "Result Slips" hazitakubaliwa.

Utambulisho: Lazima uwe na kitambulisho halali (NIDA, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Pasipoti, Leseni ya Udereva, au barua ya Serikali ya Mtaa).

Barakoa (Mask): Ni lazima kuvaa barakoa wakati wote wa usaili.

Mavazi: Wasailiwa wanatakiwa kuvaa mavazi ya heshima na nadhifu kulingana na miongozo ya utumishi wa umma.

Gharama: Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri, na malazi.

Ajira Portal: Hakikisha unakumbuka namba yako ya usaili na taarifa zako za kuingia kwenye mfumo (Email & Password) kwa ajili ya usaili wa mchujo wa kidijitali.

JINSI YA KUANGALIA MAJINA

Kuangalia orodha kamili ya majina yaliyoitwa, unaweza kupakua tangazo rasmi kupitia tovuti ya Sekretarieti ya Ajira (PSRTS) au kubofya link hapa chini:

👉 Pakua PDF la Majina ya Usaili MUST Hapa

Kama jina lako halipo kwenye orodha hii, tafadhali ingia kwenye akaunti yako ya Ajira Portal kuona sababu za kutokuitwa.

Kila la kheri kwa wasailiwa wote!

Limetolewa na:

Makamu Mkuu wa Chuo,

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Post a Comment

0 Comments