Communications & Development Manager - Honeyguide Foundation
Mwajiri: Honeyguide Foundation
Nafasi: Communications & Development Manager
Mahali: Tanzania
Aina ya Ajira: Muda wote (Full-time)
Tarehe ya Mwisho ya Maombi: 20 Septemba 2026
Kuhusu Honeyguide Foundation
Honeyguide Foundation ni taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania inayojenga ushirikiano kati ya jamii za wenyeji na sekta ya utalii kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na makazi asilia.
Kupitia mtazamo shirikishi wa ujasiriamali wa kijamii, Honeyguide inakuza mifumo ya kiuchumi inayosaidia uhifadhi na maendeleo endelevu. Taasisi hii inasisitiza utawala bora unaowezesha jamii kusimamia rasilimali za maeneo yao kwa ufanisi zaidi.
Honeyguide inatoa huduma za ushauri, ujengaji wa uwezo, na kuwezesha ushirikiano na wafanyabiashara wenye uwajibikaji ili kusaidia jamii kukabiliana na changamoto za sasa za kimazingira na kiuchumi.
Sifa Zinazohitajika (Professional Experience)
- Uzoefu wa kazi wa miaka 5–7 katika mawasiliano (communications), usimamizi wa maarifa (knowledge management), uwezeshaji wa ufadhili (fundraising support), sera (policy), maendeleo au taaluma inayohusiana.
- Uzoefu wa miaka 2–3 katika kusimamia au kuratibu timu.
- Uzoefu uliothibitishwa wa kusimamia miradi mingi na malengo yenye muda mfupi (competing deadlines).
- Uzoefu katika mashirika yasiyo ya kiserikali, uhifadhi, maendeleo, utafiti au mazingira yanayofanana ni faida (desirable).
- Uzoefu wa kufanya kazi na mawasiliano ya wafadhili, ruzuku (grants) au taratibu za ufadhili (fundraising) ni faida.
- Kuonyesha maslahi au uzoefu wa vitendo katika matumizi ya AI na zana za kidijitali.
Maelekezo ya Maombi
Waombaji wa nafasi ya Communications & Development Manager wanapaswa kuwasilisha:
1. Barua ya Maombi (Covering Letter)
Barua ya maombi ieleze:
- Kwa nini unataka kufanya kazi na Honeyguide.
- Kwa nini unaamini unafaa kwa nafasi hii.
- Uzoefu wako husika katika mawasiliano ya kimkakati, uongozi wa timu na usimamizi wa watu.
- Uzoefu wako katika kuendeleza mifumo, kuratibu kazi na kusimamia vipaumbele vingi.
- Uzoefu wako au maslahi yako katika matumizi ya AI na zana za kidijitali kuboresha mawasiliano na ufanisi wa kiutendaji wa taasisi.
2. Wasifu (CV)
Wasilisha CV yako ikionyesha uzoefu wako wa kitaaluma, sifa na ujuzi husika.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Tuma maombi yako kwa barua pepe: job@honeyguide.org
Mada ya Barua Pepe (Subject Line): Application – Communications & Development Manager
Taarifa Muhimu
| Muhimu | Usitume vyeti, transcript za kitaaluma, referees au viambatanisho vingine vyovyote katika hatua hii. Ambatanisha barua ya maombi na CV pekee. |
| Onyo | Tafadhali fuata maelekezo yote hapo juu. Kutofuata maelekezo kunaweza kusababisha maombi yako kukataliwa. |
| Tarehe ya Mwisho | 20 Septemba 2026 |
| Maelezo ya Ziada | Waombaji watakaochaguliwa tu (shortlisted) ndio watawasiliana nao. |

0 Comments