Tangazo la Kuitwa Kazini Sekretarieti ya Ajira – Septemba 09, 2026 | Majina ya Walioitwa

Tangazo la Kuitwa Kazini - Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma

Kumb. Na: JA. 9/18/01"E"/57
Tarehe ya Tangazo: 09/09/2026

Kuhusu Taasisi

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Rais, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye jukumu la kuratibu mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma, ikiwemo usaili na upangaji wa waliofaulu katika vituo vya kazi.

Maelezo ya Tangazo

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 13 Desemba 2025 na tarehe 19 Agosti 2026 kuwa matokeo ya waliofaulu usaili huo yameorodheshwa katika tangazo hili. Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Mamlaka za Ajira Zilizohusika

  • Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
  • Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
  • Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji
  • Halmashauri ya Mji wa Korogwe
  • Halmashauri ya Mji wa Makambako
  • Halmashauri ya Wilaya ya Pangani
  • Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
  • Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA)

Baadhi ya Kada Zilizoitwa Kazini

  • Admission Officer II
  • Examination Officer II
  • Accounts Officer II
  • Afisa Tawala Daraja la II
  • Artisan Grade II (Masonry and Bricklaying)
  • Estate Officer II (Civil Engineer)
  • Health Assistant I na II
  • Laboratory Engineer II (Mechanical Engineering)
  • Laboratory Technician II (Civil Engineering)
  • Library Assistant II na Library Officer II
  • Nursing Officer II / Afisa Muuguzi Daraja la II
  • Procurement Officer II
  • Public Relations Officer II
  • Records Management Assistant II
  • Tabibu Daraja la II (Clinical Officer Grade II)
  • Workshop Assistant II na Workshop Technician II
  • Fundi Sanifu Daraja la II Ujenzi (Civil Technician Grade II)
  • Mwalimu Daraja la IIIA, IIIB na IIIC (masomo mbalimbali ikiwemo Baiolojia, Kemia na Kiingereza)
  • Afisa Biashara Daraja II (Trade Officer II)
  • Msanifu Majengo Daraja la II (Architect Grade II)
  • Mteknolojia wa Radiografa Daraja II - Radiolojia
  • Msaidizi wa Hesabu Daraja la II (Accounts Assistant II)
  • Conservation Ranger III - Wildlife Management (Law Enforcement)
  • Quantity Surveyor II

Masharti na Taarifa Muhimu

  • Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi watapata BARUA zao za kupangiwa vituo vya kazi kupitia AKAUNTI zao za Ajira Portal, kwenye sehemu ya My Applications.
  • Waombaji wanapaswa kupakua na kuchapisha (Download and Print) barua hizo na kwenda nazo kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.
  • Waombaji waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ulioainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi.
  • Waombaji wanapaswa kuwa na vyeti halisi (Original Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea, ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
  • Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi au hawakufaulu usaili, hivyo wanashauriwa wasisite kuomba tena nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Tarehe ya Mwisho

Tangazo hili halikuwa na tarehe maalum ya mwisho ya kuomba, kwani ni tangazo la matokeo ya usaili na kuitwa kazini, si tangazo la nafasi mpya za kazi.

Pakua PDF Hapa

Post a Comment

0 Comments